• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Asilimia 50 ya kuku wapata chanjo

by BAJETI
August 25, 2021
in Habari
0
Share on FacebookShare on Twitter

TANZANIA ina jumla ya kuku milioni 87.7 ambapo  katika ya hao asilimia 50.9 wamepata chanjo ikiwemo ya kuzuia ugonjwa wa Ndui.

Hata hivyo wakulima wadogo walikuwa na Kuku milioni 75.1 na mashamba makubwa yakiwa na Kuku milioni 12.5.

Hayo ni kwa mujibu wa  Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 katika Ripoti ya Matokeo Muhimu kwa Sekta za mazao,mifugo na ufugaji wa samaki iliyotolewa Agosti mwaka huu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Katika Sensa hiyo ilihusisha aina mbalimbali za mifugo inayofugwa nchini wakiwemo Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, Nguruwe na Kuku.

“Idadi ya Kuku waliochanjwa nchini kwa upande wa  ugonjwa wa Mdondo/Mhepe ni 44,591,494 sawa na asilimia 50.9 ambapo kwa upande wa ugonjwa wa Gumboro walikuwa 9,903,930 na Ndui wakiwa 13,560,766.

“Taarifa inaonesha kuwa ugonjwa wa mdondo/mahepe ulichanjwa kwa kiwango cha juu zaidi (asilimia 50.9) na Gumboro kwa kiwango cha chini zaidi (asilimia 11.3) ya kuku wote waliofugwa na wakulima wadogo.

“Idadi ya kuku waliofugwa nchini ni 87,659,579,ambapo Tanzania Bara walikuwa 83,895,395 na upande wa Zanzibar kulikuwa na Kuku 3,764,184.”imefafanua taarifa hiyo.

Kuku wa kienyenji (Picha na mtandao)

Ripoti hiyo maaalum imefafanua kuwa kwa upande wa Tanzania Bara Kuku waliopata chanjo kwa ugonjwa wa Mdondo/Mhepe walikuwa 43,795285 sawa na asilimia 52.2,Gumboro 9,402,109 wakiwa ni asilimia 11.2 ambapo kwa upande wa ugonjwa wa Ndui ni 13,138,219 ikiwa ni sawa na asilimia 15.7.

“Tanzania Zanzibar Kuku waliochanjwa ugonjwa wa Mdondo/Mhepe ni 796,209 sawa na asilimia 21.2,Gumboro 501,821 ikiwa ni asimilia 13,3 huku ugonjwa wa Ndui  wakiwa 422,547 sawa na asilimia 11.2”imeongeza taarifa hiyo

Next Post

Makalla kumaliza kero ya ardhi Dar es Salaam

Daraja la Selander lakamilika asilimia 91

Korosho yaongoza uzalishaji mazao ya biashara

Korosho yaongoza uzalishaji mazao ya biashara

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In