• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Korosho yaongoza uzalishaji mazao ya biashara

by BAJETI
November 22, 2021
in Habari
0
Korosho yaongoza uzalishaji mazao ya biashara
Share on FacebookShare on Twitter

KOROSHO imetajwa kuwa ndio zao kuu la biashara lililolimwa kwa kiasi kikubwa Tanzania Bara likifuatiwa na Pamba  huku Zanzibar ikiongoza kwa Karafuu.

Mazao hayo ni miongoni mwa mazao makuu ya biashara yaliyozalishwa Tanzania katika mwaka wa Kilimo 2019/20 yakiwemo Kahawa na Chai,

Hayo ni kwa mujibu wa  Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 katika Ripoti ya Matokeo Muhimu kwa Sekta za mazao,mifugo na ufugaji wa samaki iliyotolewa Agosti mwaka huu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Ripoti hiyo ya NBS imebainisha kuwa uzalishaji wa mazao makuu ya biashara kwa Tanzania Bara ulikuwa ni tani 872,578 na Tanzania Zanzibar tani 2,447.

“Zao Kuu la Biashara lililoripotiwa kuzalishwa kwa kiasi kikubwa Tanzania Bara ni Korosho, iliyozalishwa tani 391,110, likifuatiwa na zao la Pamba tani 331,524 na Kahawa tani 82,478.

“Kwa upande wa Tanzania Zanzibar, Zao Kuu la Biashara lililozalishwa ni Karafuu, ambapo jumla ya tani 2,438 zilizalishwa”imeongeza ripoti hiyo.

 

Korosho ikiwa tayari imeandaliwa kwa matumizi ya chakula cha binadamu(Picha na mtandao)

Ripoti hiyo imeeleza kuwa jumla ya eneo lililopandwa mazao hayo ni hekta 1,311,035 ambapo hekta 1,291,751 zililimwa na wakulima wadogo na mashamba makubwa ni hekta 19,284

“Zao la korosho lilipandwa kwenye eneo la hekta 811,733 ambapo wakulima wadogo walipanda hekta 808,143 na mashamba makubwa yalipandwa hekta 3,590 ambalo ni eneo kubwa kwa mazao makuu ya biashara.

“Zao la pamba lilipandwa kwenye eneo la ukubwa wa hekta 314,601 ambapo wakulima wadogo walipanda hekta 313,370 na mashamba makubwa yalipandwa hekta 1,231,Kahawa ikipandwa hekta 157,999 huku wakulima wadogo wakipanda hekta 151,408 na mashamba makubwa hekta 6,591” imefafanua ripoti hiyo.

Uzalishaji wa zao la korosho uliongoza kwa tani 391,119  ambapo wakulima wadogo walizalisha tani 390,412 na mashamba makubwa tani 707), ikifuatiwa na uzalishaji wa zao la Pamba lililofikia tani 331,524 huku wakulima wadogo wakizalisha  tani 330,845 na mashamba makubwa tani 679.

Kwa upande wa  Kahawa ilizalishwa tani 82,478 ambapo wakulima wakubwa walizalisha  tani 75,323 na wakulima wadogo tani 7,155.

Next Post

Maziwa ya mbuzi yafikia lita milioni 25.7

Makalla amuonya mkandarasi barabara ya Makongo

Makalla amuonya mkandarasi barabara ya Makongo

Wanahabari 124 wakimbilia Mexico

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In