UZALISHAJI wa Maziwa katika mwaka wa Kilimo 2019/20 umeonesha kuwa maziwa ya mbuzi yalizalishwa hadi kufikia lita milioni 25.7 huku Zanzibar ikizalisha lita 112,800 kwa upande wa wakulima wadogo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa uagizaji wa maziwa na bidhaa zake kutoka nje ya nchi bado ni mkubwa na zinahitajika juhudi zaidi kuongeza usindikaji na kuhamasisha unywaji wa maziwa ndani ya nchi.
Hayo ni kwa mujibu wa Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 katika Ripoti ya Matokeo Muhimu kwa Sekta za mazao,mifugo na ufugaji wa samaki iliyotolewa Agosti mwaka huu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Hata hivyo ripoti hiyo imefafanua kuwa Ngo’ombe wameongoza kwa uzalishaji wa maziwa ambapo jumla ya lita bilioni 3.13 za maziwa ya wanyama hao zilizalishwa nchini.
Ripoti imeongeza kuwa kati ya hizo, lita bilioni 3.11 sawa na asilimia 99.4 zilizalishwa na wakulima wadogo na lita milioni 17.8 ikiwa ni asilimia 0.6 zilitoka katika mashamba makubwa.

Kwa upande wa uzalishaji wa maziwa ya mbuzi, jumla ya lita milioni 25.7 zilizalishwa nchini, ambapo lita milioni 25.6 zilitoka kwa wakulima wadogo na lita 12,515 kutoka mashamba makubwa.
“Uzalishaji wa maziwa kwa mwaka wa kilimo 2019/2020,Mbuzi walikuwa 25,690,876 kwa Wakulima Wadogo wa Tanzania Bara walizalisha lita 25,565,561 na Zanzibar walizalisha lita 112,800.
“Mashamba makubwa Tanzania Bara walizalisha lita 10,895 na upande wa Zanzibar walizalisha lita 1,620.”imefafanua ripoti hiyo
Kwa upande wa Ngombe walikuwa 3,130,774,084 ambapo Wakulima Wadodo Tanzania Bara walizalisha lita 3,076,489,371 na Zanzibar walizalisha lita 36,450,637 na mashamba makubwa kwa Tanzania Bara walizalisha lita 17,574,621 na upande wa Zanzibar wakizalisha lita 259,455
“Ujumbe Muhimu,uzalishaji wa maziwa ya ng’ombe umeongezeka kutoka lita 2.5 bilioni katika Sensa ya 2007/08 hadi lita 3.1 bilioni sawa na ongezeko la asilimia 24.5 Mwaka 2019/20,uzalishaji mkubwa ukitoka kwa wakulima wadogo.
“Ongezeko la maziwa ya ng’ombe linaweza kuwa limechangiwa na utekelezaji wa sera inayolenga kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya uzalishaji kibiashara na unaozingatia mahitaji ya soko ili kuongeza kipato cha wadau wa maziwa na kuboresha hali ya maisha yao”imeongeza ripoti hiyo


Discussion about this post