• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Kuku wa kisasa wafikia milioni 44.5

by BAJETI
April 8, 2023
in Habari
0
Kuku wa kisasa wafikia milioni 44.5
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

TANZANIA inakadiriwa kuwa na kuku zaidi ya milioni 83.28 ambapo kati ya hao,wa kisasa ni milioni 44.5 huku Sekta ya Mifugo ikichangia asilimia 7.4 katika Pato la Tafa.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Idara ya Uzalishaji na Masoko katika Mashamba ya Kuzalisha Mifugo iliyotolewa hivi karibuni.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kuku wa asili wanafikia milioni 38.77 ambapo Sekta ya Mifugo ilikuwa kwa asilimia tano katika mwaka 2019/2020.

“Tanzania inakadiriwa kuwa na Ng’ombe milioni 33.4,Mbuzi milioni 21.29 na Kondoo milioni 5.65.

“Aidha hapa nchini kuna kuku  milioni  83.28 kati ya hao,kuku wa asili ni milioni 38.77 ,na kuku wa kisasa ni milioni 44.5,Nguruwe milioni 2.14 na Punda 657,389 ”imefafanua taarifa hiyo

 

 

Kuku wa asili (Kinyeji)

Aidha imeongeza kuwa Sekta ya Mifugo ilikuwa kwa asilimia tano mwaka 2019/2020 na kuchangia asilimia 7.4  ya Pato la Taifa.

Kwa upande wa Ng’ombe wa Maziwa taarifa hiyo imebainisha kuwa mwaka 2019/2020 wanyama hao walifikia milioni 1.9 ambapo mitamba ya ng’ombe wa maziwa iliyozalishwa ilifikia 18,255 na kusambazwa kwa wafugaji nchini.

“Serikali inamiliki na kuendesha mashamba matano ya kuzalisha ng’ombe bora wa maziwa na kuuza kwa wafugaji wanaohitaji ng’ombe wa maziwa.

“Aidha uzalishaji wa mitamba katika mashamba haya ni mdogo ukilinganisha na mahitaji ya wafugaji hapa nchini,hivyo kuna haja ya sekta binafsi kuwekeza katika miradi ya kuzalisha mitamba na kuuza kwa jamii ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali”imefafanua taarifa hiyo

Hata hivyo lengo ni kuzalisha ndama 1,000,000 wa maziwa kwa mwaka  na hivyo kuongeza idadi ya ng’ombe walioboreshwa hapa nchini.

“Mashamba ya Serikali kwa ajili ya kuzalisha mifugo ni matano,ambayo ni Sao Hill-Iringa,Kitulo-Njombe,Mabuki-Mwanza,Ngerengere-Morogoro na Nangaramo-Mtwara”imeongeza taarifa hiyo.  

Next Post

Chanjo ya Malaria,Kifua Kikuu kuanza kuzalishwa

Vigogo wa jeshi watimuliwa

Wezi waiba chanjo ya CORONA

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In