Warning: Attempt to read property "child" on null in /home/bajetico/public_html/wp-content/themes/hilonga/class/ContentTag.php on line 45
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Sayansi na Teknolojia

Chanjo ya Malaria,Kifua Kikuu kuanza kuzalishwa

by BAJETI
August 29, 2021
in Sayansi na Teknolojia
0
Share on FacebookShare on Twitter

KAMPUNI ya utengenezaji wa chanjo ya CORONA (UVIKO-19) ya BioNTech  ya Ujeruman, inajipanga kujenga vituo vya uzalishaji wa chanjo ya ugonjwa wa Malaria na Kifua Kikuu (TB) nchini Rwanda na Senegal.

Taarifa  ya BioNTech,iliyotoewa hivi karibuni  imeeleza kuwa inachunguza kuanzisha vituo vya uzalishaji wa chanjo ya ugonjwa wa Malaria na Kifua Kikuu ya mRNA nchini Rwanda na Senegal.

Mkurugenzi Mkuu na mwanzilishi wa Kampuni hiyo ya BioNTech Prof.  Uğur Şahin,amekutana na  Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Senegal Macky Sall na Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula Von Der Leyen  huko Berlin, Mji Mkuu wa Ujerumani kuangalia mazingira ya kuanza uzalishaji wa chanjo za magonjwa hayo

Kampuni hiyo imekubali kuzalisha chanjo zenye msingi wa mRNA za Malaria na Kifua Kikuu katika Bara la Afrika.

Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa chanjo hizo,Şahin amesema lengo lao ni kujenga uwezo endelevu wa uzalishaji wa chanjo,kukuza chanjo na kuboresha huduma za matibabu barani Afrika.

Hata hivyo Sahin katika tathmini yake juu ya mpango huo, alishukuru chanjo ya BioNTech ya msingi wa MRNA kwa msaada na uaminifu.

BioNTech ilitangaza mnamo Julai mwaka huu kuwa itajaribu kutengeneza chanjo ya ugonjwa wa malaria amabo ni ugonjwa unaoambukizwa kwa kuumwa na mbu barani Afrika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Aprili 25,2021 katika siku ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria duniani,Katibu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia haipaswi kusahau  kuwa mamilioni ya watu duniani kote, wanaendelea kuugua au kufariki dunia kutokana na Malaria.

Amesema kila mwaka Malaria husababisha vifo vya watu zaidi ya 400,000, wengi wao ni watoto wadogo barani Afrika ambapo pia kila mwaka kuna zaidi ya wagonjwa wapya milioni 200 wa Malaria.

Mwaka 2019, bara la Afrika lilibeba mzigo wa asilimia 94 ya wagonjwa wote wa Malaria na vifo vitokanavyo na Malaria duniani, ambapo kati ya visa hivyo, zaidi ya nusu ni katika mataifa matano tu.

Mataifa hayo ni Nigeria asilimia 27, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), asilimia 12, Uganda asilimia tano,Niger asilimia tano na Msumbiji asilimia nne.

Mwaka 1897 Daktari wa Uingereza Ronald Ross ndiye aliyegundua kuwa mbu  jike ndio wanaoambukiza ugonjwa wa Malaria kwa binadamu.

Next Post

Vigogo wa jeshi watimuliwa

Wezi waiba chanjo ya CORONA

Zanzibar yaongoza ufugaji Mwatiko

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In