WANANCHI wa Kata ya Imbaseny wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha wametakiwa kuchangia michango kwa ajili ya maendeleo ya eneo hilo ikiwemo ujenzi wa sekondari katika eneo ili kupunguza watoto kutembea umbali mrefu.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru Jeremia Kishili wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya Kata hiyo.
Amesema katika Kata hiyo wanajenga Shule ya Sekondari ya Imbaseny ambayo wanatarajia kuifungua mwakani hivyo wananchi wanapaswa kutoa michango ya ujenzi huo na kuacha dhana potofu kuwa hawapaswi kutoa michango yeyote katika kuchangia maendeleo ya elimu.
Kishili ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Imabaeny amewaomba pia Walimu na Wafanyakazi wengine wawe mfano wa kwanza kuchangia michango ya maendeleo katika kata hiyo.
Amewataka Wananchi wa Meru kuzidi kutoa ushirikiano kati yao na Viongozi wa Kata na Vitongoji ili kuharakisha maendeleo katika jamii zao. Mbali na Sekta ya Elimu Kishili amebainisha kuwa tayari wameanza kuboresha miundombinu ya barabara ikiwemo ile ya Aloisi
Discussion about this post