Warning: Attempt to read property "child" on null in /home/bajetico/public_html/wp-content/themes/hilonga/class/ContentTag.php on line 45
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Kiini migogoro ya ardhi Dar es Salaam chafichuliwa.

by BAJETI
September 3, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema migogoro mingi ya uvamizi wa ardhi inatokana na Taasisi zinazomiliki maeneo hayo kuyatekeleza kwa muda mrefu.

Makalla ametoa kauli hiyo leo mkoani Dar es Salaam wakati wa mwendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za  Wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi ambapo leo ilikuwa zamu ya Jimbo la Mbagala.

Amesema baadhi ya Taasisi zinazomiliki maeneo hayo makubwa zimeyatelekeza kwa bila kuyaendeleza jambo linalosababisha wananchi kuingiwa na tamaa na kuweka makazi kutokana na uhaba wa maeneo.

Haya hivyo Makalla amezitaka Taasisi zote zinazomiliki maeneo makubwa ya ardhi kuhakikisha kuwa wanayaendeleza ikiwemo kuyawekea uzio ili kuondokana na uvamizi na kusababisha migogoro ya ardhi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla(aliyesimama) akizungumza na wakazi wa Mbagala (hawapo pichani) leo mkoani Dar es Salaam kuhusu utatuzi wa kero zinazowakabili(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)

Wakati huo huo ameamuru kuondolewa kwa watu wote wanaofanya biashara ndani ya eneo la Ujenzi  wa Barabara ya Mabasi yaendayo kasi  kwa kuwa inamzuia mkandarasi kufanya majukumu yake.

Makalla amelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na wafanyabiashara katika  eneo la Mbagala Rangi Tatu  kufanya biashara zao katika eneo la mradi huo licha ya ujenzi kuendelea.

Makalla ametoa agizo hilo leo  Mbagala mkoani Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi  katika majimbo yote akiwa na lengo la kuondoa migogoro hasa ya ardhi.

Amesema watu wanaofanya shughuli zao ndani ya eneo la mradi mbali na kumzuia Mkandarasi kufanya kazi zake pia wafanyabiashara hao wanahatarisha usalama wao.

Next Post

Utafiti:Uchafuzi wa mazingira kufupisha umri wa kuishi

Umasikini wakithiri Lebanon

Serikali kujenga Kituo cha Ukuzaji Viumbe Maji

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 13,061
  • Total page views 14,806

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In