• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, January 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Utafiti:Uchafuzi wa mazingira kufupisha umri wa kuishi

by BAJETI
September 3, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter
UCHAFUZI  wa Mazingira unaofikia viwango vya juu nchini India unaweza kufupisha muda wa kuishi wa mamilioni ya watu kwa kipindi cha hadi miaka tisa. Kulingana na taarifa za Shirika la Habari la CNN, utafiti uliochapishwa na Chuo Kikuu cha Sera ya Nishati cha Chicago (EPIC) umebainisha kwamba idadi yote ya Wahindi ambayo ni takriban bilioni 1.3 wanakabiliwa na kiwango hatari cha uchafuzi wa mazingira unaozidi wastani wa uchafuzi uliowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Katika utafiti huo umeripotiwa kuwa uchafuzi wa hewa ulikuwa mbaya zaidi katika Jimbo la Maharashtra eneo la Magharibi mwa Nchi na Madhya Pradesh katikati mwa nchi. Katika utafiti huo, imekadiriwa kuwa uchafuzi wa hewa, ambao umefikia viwango vya hatari sana nchini India, unaweza kupunguza muda wa kuishi wa mamilioni ya watu kwa kipindi cha hadi miaka tisa. Utafiti huo, ambao umebainisha kuwa kiwango cha uchafuzi wa mazingira huko New Delhi, Mji Mkuu wa India, pia uko juu zaidi, Utafiti huo umeonesha kuwa kiwango cha uchafuzi wa hewa kinaweza kuongezeka kwa matarajio ya maisha ya wakazi wa New Delhi hadi miaka 10, kadiri ukubwa wa uchafuzi wa hewa unavyopungua kwa vigezo vya WHO. Kulingana na utafiti wa EPIC, uchafuzi wa hewa nchini India unakadiriwa kufupisha muda wa kuishi wa takriban watu milioni 520, ambayo inalingana na asilimia 40 ya idadi ya watu nchini. Awali kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliofanywa wa hali ya hewa duniani ‘State of Global Air 2020’ ambapo India na nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika zinaongoza. Kwa mujibu wa utafiti huo, miongoni mwa watoto wadogo karibu 500,000 waliopoteza maisha chini ya mwezi mmoja baada ya kuzaliwa kutokana na uchafuzi wa hali ya hewa mwaka jana, 116,000 mongoni mwao ni wa India, huku zaidi ya vifo 236,000 vikiripotiwa katika nchi za chini ya jangwa la Sahara. Kwa ujumla, waliofariki dunia kote duniani mwaka 2019 kutokana na uchafuzi wa hali ya hewa kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na taasisi za Health Effects Institute (HEI) na Institute for Health Metrics and Evaluation’s Global Burden of Disease za Marekani, ni watu milioni 6.7                
Next Post

Umasikini wakithiri Lebanon

Serikali kujenga Kituo cha Ukuzaji Viumbe Maji

Watakiwa kutumia njia za asili kukabiliana na wanyamapori

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:25
  • Today's page views 25
  • Total visitors 13,182
  • Total page views 14,928

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In