• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Watakiwa kutumia njia za asili kukabiliana na wanyamapori

by BAJETI
April 18, 2024
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

 

NA MIRIAM SARAKIKYA,ARUSHA

WAKULIMA nchini wametakiwa kutumia njia za asili katika kuzuia wanyamapori kuharibu mazao yao wakati Serikali ikichukua hatua madhubiti katika kupambana na wanyama hao.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha Zainabu Makwinya wakati akitoa ufafanuzi  katika Kikao cha Baraza la Madiwani baada ya kuibuka kwa hoja za wanyamapori kuvamia mashamba ya wananchi zilizotolewa na baadhi ya madiwani.

Amesema Serikali inaendelea  kufuatilia  fedha za fidia za wakulima  wa halmashauri hiyo   ambao mazao yao  yaliharibiwa na wanyamapori.

Makwinya amefafanua kuwa  ulipwaji wa fidia kwa Wakulima 30   wa Kata ya Songoro unafuatiliwa kwani awali wananchi wengine   walipatiwa fidia pasipo kufuata utaratibu  wa kutoa taarifa kwa viongozi  na nyingine ambazo zinapakana na maeneo ya Hifadhi ya Wanyamapori.

Makwinya ameahidi kutembelea maeneo yaliyo mpakani na hifadhi ili kuweka vizuizi  vya asili ambavyo vitawazuia wanyamapori  wakali kushambulia mazao ya Wakulima.

Awali baadhi ya madiwani wamesema pamoja na wakulima hao kupata hasara ya mazao yao kila mara Serikali imekua ikitoa fidia pasipo kutoa taarifa kwa viongozi wa maeneo husika hivyo fidia hiyo haiwafikii walengwa wote.

Diwani wa Kata ya Ngarinanyuki Aminieli Mungure ameiomba Serikali kufuata utaratibu wa kutoa fidia hizo ili kuhakikisha zinawafikia walengwa wote

Naye Afisa Maliasili na Utalii wa Halmashauri hiyo Charles Mungure amesema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuzuia mazao yao kushambuliwa na wanyamapori

Amesema ni vizuri kwa wananchi kutowauwa wanyamapori wanaovamia mashamba yao na kutoa taarifa sehemu husika lakini kuwauwa ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Next Post

Sensa yaibua Vikwazo Sekta ya Kilimo

DC aagiza kutengwa siku kusikiliza kero za wananchi.

Washerekea wafungwa kutoroka gerezani

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In