SEKTA ya Kilimo nchini inakabiliwa na vikwazo zaidi ya 20 ikiwemo migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na upatikanaji wa mikopo.
Hayo ni kwa mujibu wa Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 katika Ripoti ya Matokeo Muhimu kwa Sekta za mazao,mifugo na ufugaji wa samaki iliyotolewa Agosti mwaka huu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Ripoti hiyo ya NBS imebainisha matokeo ya Sensa yanaonesha kuwa, kaya nyingi zilikutana na vikwazo mbalimbali katika Mwaka wa Kilimo 2019/20.
Ripoti hiyo imebainisha kuwa kati ya vikwazo vingi vilivyoripotiwa na kaya katika shughuli za kilimo ni mabadiliko ya tabianchi (ukame, mafuriko, gharama za pembejeo, upatikanaji wa ardhi, bei ndogo za mazao, magonjwa na wadudu waharibifu, upatikanaji wa pembejeo na rutuba ya udongo.
Vikwazo vingine ni pamoja na Umiliki wa Ardhi,Upatikanaji wa mbegu bora,Uharibifu wa wanyama na ndege,Nyingine,Huduma za ugani,Upatikanaji wa mikopo,Upatinakaji wa soko na taarifa za masoko,Wizi wa mazao.
“Upatikanaji wa maji kwa matumizi ya binadamu,Upatikanaji wa dawa za mifugo,Mapato nje ya shughuli za kilimo,Migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji,Gharama za usafirishaji,Vifaa vya umwagiliaji na Uvunaji”imefafanua ripoti hiyo
Hata hivyo,ripoti hiyo imehitimisha kwa kueleza kuwa Kilimo kimeendelea kufanywa kwa kiasi kikubwa na wakulima wadogo kwenye maeneo yote ambayo ni uzalishaji wa mazao, ufugaji wa mifugo na samaki kwa tija ndogo na uzalishaji umeongezeka kwa sababu ya upanuzi wa eneo linalolimwa.
“Tija ya uzalishaji kwa wakulima wakubwa ni kubwa, na katika mnyororo wa thamani wanapata mara mbili zaidi ya wakulima wadogo, na Mabadiliko ya hali ya tabianchi imeripotiwa kuwa ni moja ya kikwazo kikuu kwa Sekta ya Kilimo.”imeongeza ripoti hiyo.
Discussion about this post