• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Wakulima wakwepa mbolea ya viwandani

by BAJETI
September 7, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

MATUMIZI ya Mbolea ya Viwandani yameonesha kushuka katika Mwaka wa Kilimo 2019/20 hali inayoweza kuchangiwa na bei ya bidhaa hiyo kutokana na  kuagizwa kutoka nje ya nchi.

Hata hivyo Mbolea za Asili zimekuwa zikitumika zaidi ikilinganishwa na Mbolea za Viwandani katika uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini.

Hayo ni kwa mujibu wa  Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 katika Ripoti ya Matokeo Muhimu kwa Sekta za mazao,mifugo na ufugaji wa samaki iliyotolewa Agosti mwaka huu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Hata hivyo ripoti hiyo imefafanua kuwa  katika mwaka wa Kilimo 2019/20, jumla ya hekta milioni 2.8 sawa na asilimia 20.1 ya eneo lililopandwa ziliwekwa mbolea.

Kati ya hizo, hekta milioni 2.7 ni kutoka Tanzania Bara na hekta 40,020  kutoka Zanzibar ambapo asilimia 60.6 ya eneo lililopandwa lilitumia mbolea za asili na asilimia 39.4 mbolea za viwandani.

“Eneo lililowekwa Mbolea Tanzania ni hekta Milioni 2,762,729,Tanzania Bara hekta Milioni 2,722,709 na Tanzania Zanzibar hekta 40,020 ambapo eneo lililowekwa mbolea ya asili Tanzania ni hekta Milioni 1,673,211 ambapo Tanzania Bara hekta Milioni 1,655,311 na Tanzania Zanzibar ni hekta 17,900.

“Eneo lililowekwa Mbolea ya Viwandani Tanzania ni hekta Milioni 1,089,517 ambapo Tanzania Bara ilikuwa hekta Milioni 1,067,398 na Tanzania Zanzibar ni hekta 22,119”imeonesha ripori hiyo

Mbolea ya asili (picha na mtandao)

Hata hivyo ujumbe muhimu wa ripoti ni kuwa kumekuwa na matumizi madogo ya mbolea katika uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini.

Kwa upande wa uhusiano wa kisera ripoti hiyo imeeleza kuwa  licha ya kuhimizwa kwa matumizi ya mbolea, bado mwitikio wa matumizi ni mdogo.

“Hali hii inaweza kuwa inachangiwa na bei kubwa za mbolea ya viwandani ambayo huagizwa kutoka nje ya nchi.

“Sera zilenge kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vya kuzalisha mbolea nchini ili kupunguza bei zake na hivyo kuvutia wakulima wengi kuzitumia.”imebainisha ripoti hiyo

Hata hivyo ripoti hiyo imeongeza kuwa matumizi makubwa ya Mbolea za Asili yanatoa fursa ya kutafuta masoko maalum ambayo yana utayari wa kulipia bei kubwa kwa mazao yaliyozalishwa kwa Mbolea za Asili.

Next Post

Watu tisa kati ya 10 hupumua hewa iliyochafuliwa

Jeshi lawaachia wafungwa wa kisiasa

Serikali kuwapatia makazi Kaya 644 Magomeni Kota

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In