KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa watu 9 kati ya 10 wanapumua hewa iliyochafuliwa, hali ambayo kila mwaka inasababisha vifo vya mapema vya watu milioni 7.
Amesema kati ya hao watoto ni 600,000 na kuhimiza kuchukuliwa hatua madhubuti kutatua changamoto hiyo sasa ili kuzuia idadi ya vifo isiongeze ifikapo mwaka 2050.
Guterres ametoa kauli hiyo jijini New York nchini Marekani wakati wa maadhimisho ya Siku ya Hewa Safi na Anga ya Bluu ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Septemba 9.
Hata hivyo Guterres katika taarifa yake amekumbusha kuwa uchafuzi wa hali ya hewa ni “dhihirisho la wazi la ukosefu wa usawa ulimwenguni,” kwani vifo vingi vinavyohusiana na janga hili hufanyika katika nchi za kipato cha chini na cha na kati na katika vitongoji masikini vya mataifa tajiri.
“Umaskini unalazimisha watu kuishi karibu na vyanzo vya uchafuzi wa mazingira, kama vile viwanda na barabara na pia husababisha watu Bilioni tatu wanaendelea kutumia mafuta kisukuku au mafuta ya taa kwa kupikia na kwa kupasha nyumba joto na kuwasha taa”amebainisha Guterres.
Aidha amefafanua kuwa uchafuzi wa mazingira sio tu unaharibu afya za binadamu, lakini pia unachangia kuongeza shida ya hali ya hewa,
“Katika siku hii ya kimataifa ya hewa safi kwa anga ya bluu, ninahimiza nchi zote kufanya bidi zaidi ili kuboresha hali ya hewa na Sheria ya kitaifa inayotegemea ushahidi inaweza kusaidia kutekeleza miongozo juu ya ubora wa hewa iliyowekwa na Shirika la afya duniani”ameeleza Guterres.
Wakati huo huo, Guterres ametaka kuwe na viwango vikali vya kudhibi kuchafua hewa kunakotokana na magari, mitambo, ujenzi na viwanda, kuondoa matumizi ya makaa ya mawe na kuwekeza katika nishati mbadala badala ya mafuta kisukuku(mafuta ya taa).
“Ikiwa tutachukua hatua hizi, tunaweza kuokoa hadi maisha ya watu milioni 150 katika karne hii na kusaidia kusafisha mazingira yetu,” ameongeza Guterres
Discussion about this post