NYOTA wa zamani wa klabu ya Simba Sphere Mbwembwe pamoja na mashabiki wa klabu hiyo wameandaa michuano ya mchezo wa mpira wa miguu katika Jimbo la Seregerea jijini Ilala Mkoa wa Dar es Salaam lengo likiwa ni kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana.
Michuano hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Segerea Super Cup’ imeanza kutimua vumbi juzi ndani ya Uwanja wa Dogodogo kwa ikijumuisha timu 16 ambazo zitashiriki michuano hiyo.
Mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo ulichezwa kati ya Songea FC wakikabiliana na Segerea FC ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo.
Hata hivyo katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo mkoani Dar es Salaam leo,mgeni rasmi katika uzinduzi huo Hope Kaiza, asema amevutiwa na mawazo ya wadau hao wa soka na kwamba ataunga mkono kuhakikisha Segerea inakuwa na vipaji vya kutosha.
Kaiza ambaye pia ndio Mdhamini Mkuu wa michuano hiyo amesema kwa sasa mpira ni ajira kubwa kwa vijana hivyo wanatakiwa kuwekezewa ili kutumiza ndoto zao.
“Niko kwa hapa kwa sababu nina mapenzi na mpira hivyo nitakuwa nawasapoti vijana kwa kile nilichonacho,hii itasaidia vijana wa Segerea lakini pia Tanzania kwa ujumla kwa kuwa Kijana yeyote atakae pata mafanikio ni kwa ajili ya Taifa zima.
“Jambo la msingi wazingatie malengo Kama wazazi na wadau tumeamua kujitoa kwa ajili yao nao wapambane ili kufukia ndoto zao,” amesema Kaiza.
Aidha Kaiza amefafanua kuwa katika michuano hiyo kutakuwa na zawadi mbali ambazo zitatolea huku mshindi wa kwanza akichukua mbuzi na wa pili jezi na mashabiki watakao shangilia vizuri.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo Shebi Machumani amebainisha kuwa Tanzania kuzalisha wachezaji wakubwa kila siku kazi hiyo haipo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pekee bali wadau ndio wanatakiwa kuongeza nguvu katika maeneo yao ili kuibua vipaji.
“Nashukuru Mungu kwanza maandalizi yalikuwa mazuri na wachezaji wote ambao wapo hapa wanaujua mpira naimani msimu ujao baadhi yao wataweza pata nafasi katika klabu mbalimbali,” ameongeza Machumani
Discussion about this post