• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 25, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Serikali kumaliza mgogoro Msitu wa Pugu Kazimzumbwi

by BAJETI
September 11, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amesema  azma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kutatua migogoro iliyodumu kwa muda mrefu ukiwemo wa Msitu wa Pugu Kazimzumbwi na wananchi.

Amesema ni lazima migogoro kama hiyo ifike mwisho  kwa kuwa kudumu kwa muda mrefu kwa migogoro hiyo kunarudisha nyuma maendeleo.

Makalla ameyasema hayo jijini Ilala Mkoa wa Dar es Salaam  wakati wa ziara ya kusikiliza kero na kutatua migogoro ya wananchi ambapo leo ni zamu ya Jimbo la Ukonga

Amesema  ni muhimu mgogoro wa Msitu wa Pugu  Kazimzumbwi ufike mwisho na kuwataka Wakala wa Huduma za  Misitu Tanzania(TFS) kupunguza matumizi makubwa ya nguvu.

“Azma ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kushughulikia migogoro ya wananchi, sasa tutakutana na Wizara tatu za Ofisi ya Rais Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ardhi ili kupata ufumbuzi”amesema Makalla.

Makalla amefafanua kuwa wakati anaendelea kushughulikia mgogoro huo ni vyema TFS ikashirikiana na Wananchi hao na kuongeza kuwa ni marufuku vitendo vya kukamata Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam kuwapeleka Wilaya ya Kisarawe mkoani wa Pwani.

Miongoni mwa vilio vya wananchi hao ni matukio ya kupigwa, kuteswa na kukamatwa kwa Wakazi wanaozungukwa na Msitu huo.

Mkuu wa Mkoa wa Darb es Salaam Amos Makalla (Kulia)

Hata hivyo TFS imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa Misitu inalindwa na kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria hali inayofanya kuendelea kuonekana hadi sasa na baadhi ya misitu kutumika kama sehemu ya utalii na kuhifadhi wanyama,wadudu na uoto wa asili.

Licha ya juhudi hizo lakini pia baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wa mazao ya Misitu wamekuwa chanzo cha TFS kutumia nguvu kuwadhibiti kutokana na kuharibu misitu kwa kujiangalia wao binafsi na si ya Taifa na vizazi vijavyo.

Next Post

Wazazi shirikianeni na walimu kutimiza malengo ya wanafunzi

Askofu Kitoi:Tumieni muda vizuri kujiletea maendeleo

Nyoka wasababisha vifo vya watu 137,000

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:15
  • Today's page views 15
  • Total visitors 16,469
  • Total page views 18,680

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In