• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Wazazi shirikianeni na walimu kutimiza malengo ya wanafunzi

by BAJETI
September 13, 2021
in Habari
0
Share on FacebookShare on Twitter

WAZAZI  nchini wametakiwa kushirikiana na Walimu na wakiwemo walezi wengine wa Shule  kuhakikisha kuwa watoto wanafanya vizuri na kutimiza malengo waliyojiwekea katika elimu.

Mbali na hilo lakini pia Walimu wametakiwa  kuwapeleka wanafunzi katika mitihani ya ujirani mwema ili kuwajengea uwezo wa kufanya vizuri katika masomo yao.

Akizungumza katika mahafali ya Tano ya  Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Tumaini Mistion iliyopo wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha, Mkurugenzi   wa Shule ya Msingi  Mecsons  Mecky Shirima amesema ni muhimu kwa Wazazi kushirikiana na Walimu kwa kuwa jambo hilo hutengeneza mazingira mazuri baina ya pande hizo mbili hali inayosaidia wanafunzi kufanya vizuri.

Amesema ni muhimu kwa Walimu pia kuwapeleka wanafunzi katika mitihani ya ujirani mwema ili kuwajengea uwezo wa kufanya vizuri katika masomo yao.

Amesema kufanyika hivyo kunajenga uwezo kwa mwanafunzi kujiamini katika kufanya mitihani yake ya mwisho hali inayoongeza ufauli zaidi.

Hata hivyo Shirima amewataka  wahitimu  kutambua kuwa Elimu haina mwisho  hivyo wanapaswa kusoma kwa bidii kutokana na kukuwa kwa Sayansi na Teknolojia.

Mkuu wa Shule ya Msingi Tumaini Mistion iliyopo wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha Namnyaki Mollel akisoma taarifa ya maendeleo ya shule hiyo kwa wazazi na wanafunzi (hawapo pichani)wakati wa mahafali ya tano ya Darasa la Saba yaliyofanyika hivi karibuni(Picha na mpigapicha wetu)

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Namnyaki Mollel amesema wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa  wakifanya mitihani ya ujirani mwema ambayo wamekuwa wakifanya kwa shule zilizopo ndani ya mkoa na hata nje ya Mkoa wa Arusha.

Amesema kuwa shule hiyo inatarajia kuanzisha Sekondari  pamoja na vyuo vya ufundi kwa faida za vizazi vijavyo.

Mwalimu Namnyaki  amewasihi wahitimu hao  kutojihusisha na makundi yeyote mabaya ambayo yatazima ndoto zao katika elimu na badala yake wawe mabalozi Waziri ndani ya jamii.

Next Post

Askofu Kitoi:Tumieni muda vizuri kujiletea maendeleo

Nyoka wasababisha vifo vya watu 137,000

Serikali yataka uhuru wa kisera kwa nchi zinazoendelea

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 13,056
  • Total page views 14,801

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In