• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, April 20, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Serikali yataka uhuru wa kisera kwa nchi zinazoendelea

by BAJETI
September 17, 2021
in Habari
0
Share on FacebookShare on Twitter

SERIKALI  imetaka kuwepo na uhuru wa kisera kwa  nchi zinazoendelea na maskini ili kujihami na athari za uingizwaji wa bidhaa za kilimo kutoka nchi zilizoendelea.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara,Prof.Kitila Mkumbo  Septemba 16, 2021, mkoani Dar es Salaam katika Mkutano wa Mawaziri wa  Kundi la Nchi 33 (G33) wa wanachama wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) uliofanyika kwa njia ya mtandao ambapo aliongoza ujumbe kutoka Tanzania.

Kundi hilo linajumuisha nchi wanachama zenye maslahi yanayofanana ya kutaka uwazi na manufaa katika majadiliano ya WTO yanayohusu Kilimo ambapo lengo la mkutano ni kujadili na kuweka msimamo wa pamoja katika maeneo ya kipaumbele kwenye kilimo.

“Msimamo wa Tanzania ni kuwa na makubaliano ya WTO yanayokataza na kuweka vikwazo kwa nchi zilizoendelea wanachama wa Shirika hilo kutoa misaada kwa wazalishaji wao inayoathiri biashara za nchi nyingine wanachama.

“Hii ni pamoja na kutaka uwepo uwazi kwa  nchi zilizoendelea kwa mfano katika utoaji ruzuku kwa wakulima wao,”amesema Prof.Mkumbo.

Prof Mkumbo amefafanua kuwa Tanzania imesisitiza kutaka nchi zinazoendelea na maskini (Developing and Least Developing Countries-LDCs) wanachama wa WTO kuwa na uhuru wa kuhifadhi chakula kwa madhumuni ya usalama wa chakula.

Mwenyekiti wa Kundi la Nchi 33 (G33) Wanachama wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) ambaye pia ni Waziri wa Biashara wa Indonesia My Muammad Lutfi akiongoza mkutano huo kwa njia ya mtandao (Picha na mpigapicha wetu ).

Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti My Muammad Lutfi ambaye ni Waziri kutoka nchini  Indonesia anayesimamia biashara.

Mbali na Mwenyekiti huyo lakini pia mkutano huo  ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa WTO, Ngozi Okonjo-Iweala na ulikuwa sehemu ya maandalizi ya nchi hizo katika Mkutano wa 12 wa ngazi ya juu wa maamuzi wa WTO (MC12) unaotarajiwa kufanyika mjini Geneva, Uswisi mwezi Desemba 2021.

Next Post
Wanawake waongoza kumiliki silaha Marekani

Wanawake waongoza kumiliki silaha Marekani

TAIWAN kuipatia Japan mitungi 1000 ya gesi kupambana na UVIKO-19

Wazazi waacheni watoto wasome fani wazipendazo

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:20
  • Today's page views 33
  • Total visitors 15,815
  • Total page views 17,923

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In