• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Wanawake waongoza kumiliki silaha Marekani

by BAJETI
November 22, 2021
in Habari
0
Wanawake waongoza kumiliki silaha Marekani
Share on FacebookShare on Twitter

UTAFITI uliofanywa nchini Marekani umeonesha kuwa wanawake wanaongoza kumiliki silaha za moto kuliko wanaume kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vurugu za uchaguzi wa rais wa nchi hiyo uliofanyika mwaka 2020

Utafiti wa kitaifa kuhusu hali ya umiliki wa silaha za moto katika mwaka huu wa 2021 uliofanywa na wataalamu wa Kitivo cha Afya ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard nchini humo  umeonesha kuwa, kuanzia Januari 2019 hadi Aprili mwaka huu, wanawake wapatao milioni 5.3 wa Kimarekani wamenunua silaha kwa mara ya kwanza.

Karibu wanaume milioni nne wa nchi hiyo, nao pia walinunua silaha katika kipindi hicho.

Mtafiti wa Kitivo hicho Afya ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard, Dk.Deborah Azrael amesema utafiti wao, walichunguza rekodi za watu 19,000 na kwamba huo ulikuwa utafiti mpana na jumuishi zaidi kitaifa kufanywa nchini Marekani kuhusiana na ununuzi wa silaha.

Amesema sababu ya kuongezeka idadi ya wanawake wanaonunua silaha nchini Marekani ni kutokana na ugonjwa wa  UVIKO-19, malalamiko ya kijamii, yakiwemo yale yaliyogubikwa na machafuko kufuatia mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd yaliyofanywa na askari polisi wa jimbo la Minnesota, na  machafuko ya uchaguzi wa rais wa nchi hiyo wa mwaka 2020.

Hata hivyo Utafiti  huo umeonesha pia kuwa, asilimia 55 ya wanunuzi wapya wa silaha nchini humo ni wazungu, asilimia 21 ni Wamarekani weusi na asilimia 19 ni wale wenye asili ya Latini.

Kwa upande wa wanunuzi wanawake, Wamarekani weusi wanaunda asilimia 28 tu ya wanunuzi hao wa silaha za moto.

Next Post

TAIWAN kuipatia Japan mitungi 1000 ya gesi kupambana na UVIKO-19

Wazazi waacheni watoto wasome fani wazipendazo

Magugu maji yatishia uhai wa Ziwa Jipe

Magugu maji yatishia uhai wa Ziwa Jipe

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In