• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, March 8, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Magugu maji yatishia uhai wa Ziwa Jipe

by BAJETI
November 22, 2021
in Mazingira
0
Magugu maji yatishia uhai wa Ziwa Jipe
Share on FacebookShare on Twitter

MBUNGE  wa Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro Joseph Tadayo ameiomba serikali kusaidia changamoto ya kuondoa magugu maji katika Ziwa Jipe kutokana na eneo kubwa kumezwa na majani hayo.

Ziwa hilo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 30,lipo hatarini kutoweka kutokana na eneo kubwa la ziwa hilo kumezwa na magugu maji.

Ombi la Mbunge huyo limetolewa  leo wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Hamad Chande ya kukagua hali ya ziwa hilo.

Tadayo  amesema licha ya wao kufanya juhudi za kupambana na magugu hayo lakini ni muhimu pia kwa serikali ikaongeza nguzu zaidi kutokana na ziwa hilo kutegemewa kwa shughuli mbalimbali ikiwemo Uvuvi wa Samaki,Mradi mkubwa wa Maji katika Wilaya ya Same, Mwanga,Korogwe pamoja na miradi mikubwa ya Kilimo cha Umwagiliaji.

“Ziwa hilo lina umuhimu sana kutokana na miradi mikubwa ya uzalishaji wa umeme,miradi ya maji na kilimo zinategemea ziwa hili na endapo hatua za haraka hazitachukuliwa miradi yote inayotegemea maji kutoka ziwa hilo zitakufa,”amesema Tadayo

Amefafanua kuwa kikubwa kinachotakiwa ni kuondoa yale magugu maji ili wananchi waendelee na shughuli zao za Uvuvi  na Halmashauri kuendelea kupata mapato yanayotokana na uvuvi.

Amebainisha kuwa  Ziwa hilo litasaidia kuongeza ajira kwa vijana na kunufaisha wakazi zaidi ya 2564 wanaolizunguka pamoja na baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Moshi vijijini.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Chande amesema kutoweka kwa ziwa jipe kunaweza kukawa na madhara makubwa kwa Taifa na kupoteza fursa za uwekezaji kwa wananchi.

Hata hivyo Chande alimtaka Tadayo kushirikiana kwa pamoja ili waweze kuondoa magugu hayo ndani ya ziwa hilo ili liendelee kutoa huduma kwa wananchi wa jimbo hilo na Wilaya zingine kwa vizazi vya sasa na vijavyo

Next Post
Guterres:Ulimwengu hauelekei kufikia malengo vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa

Guterres:Ulimwengu hauelekei kufikia malengo vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa

Nderiananga:Wafichueni watoto wenye ulemavu wa kusikia

Kampeni ya changia damu kuokoa maisha yaanza kwa kishindo

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:16
  • Today's page views 16
  • Total visitors 14,898
  • Total page views 16,756

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In