• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Guterres:Ulimwengu hauelekei kufikia malengo vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa

by BAJETI
November 22, 2021
in Mazingira
0
Guterres:Ulimwengu hauelekei kufikia malengo vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa
Share on FacebookShare on Twitter

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake kwamba ulimwengu hauelekei kufikia malengo kadhaa ya dharura katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini New York nchini Marekani,Guterres amesema kulingana na ahadi za sasa za nchi wanachama, ulimwengu uko kwenye hali mbaya ya kufikia nyuzi 2.7 Celsius za joto, badala ya nyuzi 1.5 Celsius ambayo wote walikubaliana iwe kikomo.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika,Guterres amesema sayansi inawaambia kuwa kitu chochote kilicho juu ya nyuzi 1.5 kitakuwa janga,

“Ninaamini bado kuna kazi kubwa ya kufanya kuhusiana na kupunguza gesi chafu na karibu asilimia 80 ya gesi chafu ni kutoka mataifa tajiri ya kundi la G20”amesema Guterres

Umoja wa mataifa unasema, ili kufikia nyuzi 1.5 mataifa tajari yanapaswa kuwekeza dola billioni 100 kwa mwaka kati ya hivi sasa na mwaka wa 2025.

Uzalishaji wa gesi chafu pia unatakiwa kupunguzwa kwa asilimia 50 ifikapo mwaka wa 2030 kufikia lengo la kuwa na hewa safi ya carbon mwaka wa 2050.

Hii inajumuisha kazi ngumu ya kuzishinikiza nchi kuachana na viwanda vya mkaa wa mawe ambavyo vinachafua mazingira.

Mwezi Novemba, mataifa ya dunia yatakutana mjini Glasgow nchini Scotland kwenye mkutano muhimu wa kutathmini hatua iliyopigwa kwenye ahadi zilizotolewa tangu usainiwe mkataba wa Paris wa mwaka wa 2015 kuhusu hali ya hewa

 

Next Post

Nderiananga:Wafichueni watoto wenye ulemavu wa kusikia

Kampeni ya changia damu kuokoa maisha yaanza kwa kishindo

TRC yasafirisha tani 800 za mbolea kuelekea Kigoma

TRC yasafirisha tani 800 za mbolea kuelekea Kigoma

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In