• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

TRC yasafirisha tani 800 za mbolea kuelekea Kigoma

by bajeti
November 14, 2021
in Habari
0
TRC yasafirisha tani 800 za mbolea kuelekea Kigoma
Share on FacebookShare on Twitter

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limeendelea kuboresha huduma zake za usafirishaji wa abiria na mizigo baada ya kufunga behewa zaidi ya 20 zikiwa na mbolea kuelekea mkoani Kigoma.

Mbolea hizo kutoka Kampuni ya Yara zinazofikia zaidi ya tani 800 zinasafirishwa kutoka mkoani Dar es Salaam kuelekea Kigoma katika kuhakikisha kuwa msimu wa Kilimo wakulima hawawezi kukosa bidhaa hiyo.

Akizungumzia hali ya usafirishaji wa mizigo na abiria katika Shirika hilo mkoani Dar es Salaam jana,Meneja wa TRC Kanda ya Dar es Salaam Jonas Afumwisye amesema TRC haisafirishi abiria pekee bali hata mizigo mikubwa katika hali ya usalama zaidi na kwa wakati mmoja.

Amesema ni muhimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabishara kulitumia shirika hilo kusafirisha mizigo yao kwa uhakika kutokana na maboresho mbalimbali yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika ili kutoa huduma kwa ufanisi.

“TRC inauwezo wa kubeba mzigo mkubwa kwa wakati mmoja na hapa tuna treni yenye mabehewa zaidi ya 20 yakiwa na tani zaidi ya 800 za mbolea kueleka Kigoma.

“Mzigo huu kama ungetumia barabara basi malori zaidi ya 40 yangetumika kuusafirisha lakini kwa sisi tunausafirisha kwa pamoja na kwa wakati hivyo tunawakaribisha wadau wengine kutumia TRC kusafirisha mizigo yao”amesema Afumwisye

Mabehewa ya mizigo ya Shirika la Reli Tanzania (TRC)

Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumzia  kuboreshwa kwa TRC wamesema kutumia usafiri wa treni kusafirishia mizigo kunasaidia pia utunzaji wa barabara  kwa kuwa tani hizo ni nyingi  na yangetumika malori mengi kusafirishia mizigo huo.

Mkurugenzi wa TRC Masanja Kadogosa amekuwa akisimamia kikamilifu shughuli za shirika hilo ili kuhakikisha kuwa linatoa huduma bora na za kisasa katika kuhakikisha kuwathamani ya fedha za walipa kodi zinatumika kama inavyokusudiwa.

Next Post
Mtambo achangia ujenzi Zahanati ya Kijiji Dondo

Mtambo achangia ujenzi Zahanati ya Kijiji Dondo

Watu bilioni 2.6 hawana fursa kupata nishati safi ya kupikia

Watu bilioni 2.6 hawana fursa kupata nishati safi ya kupikia

Serikali  yaandaa mpango-kazi kuondoa matumizi  ya  Zebaki

Serikali yaandaa mpango-kazi kuondoa matumizi ya Zebaki

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In