• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, January 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

Jeshi lawaachia wafungwa wa kisiasa

by BAJETI
September 8, 2021
in Siasa
0
Share on FacebookShare on Twitter

KATIKA hali isiyotarajiwa viongozi wa kijeshi waliofanya mapinduzi nchini Guinea wamewaachia huru wapinzani wote wa kisiasa wa rais aliyepinduliwa Alpha Conde.

Kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa kumekuja wakati ambapo Jeshi la nchi hiyo kupitia Kikosi Maalum lilifanya mapinduzi siku ya jumapili na kuchukua madaraka hali iliyolaaniwa na Jumuia za Kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa

Hata hivyo shangwe zililipuka katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ukiwemo Mji Mkuu Conakry  kwa wananchi kushangilia kitendo hicho cha jeshi kwa kufanya maandamano wakiwa karibu na wanajeshi wanaofanya doria mitaani kuwaunga mkono.

Wananchi wa Guinea wakiwashangilia wanajeshi wa nchi hiyo waliokuwa wakifanya doria mitaani mara baada ya kuipindua serikali iliyochaguliwa na wananchi chini ya aliyekuwa Rais Alpha Conde hivi karibuni(Picha na mtandao)

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Ufaransa AFP liliwashuhudia baadhi ya  wafungwa wapatao 20 wakiachiwa kutoka gereza la mjini Conakry.

Mawakili wanaowatetea wafungwa hao wamesema watu 79 wamekamilisha mchakato wa kuachiwa huru kufuatia mazungumzo na viongozi wa jeshi.

Uamuzi huo umechukuliwa huku Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ikijiandaa leo kujadili mzozo uliojitokeza katika nchi hiyo.

Mapinduzi ya Jumapili yamekosolewa na Marekani, Umoja wa Ulaya na ECOWAS. Urusi nayo imetaka taasisi zote za Guinea ziruhusiwe kufanya kazi haraka iwezekanavyo.

Next Post

Serikali kuwapatia makazi Kaya 644 Magomeni Kota

Nyota Klabu ya Simba kuibua vipaji Segerea

Marekani hatarini kufilisika

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:15
  • Today's page views 15
  • Total visitors 13,172
  • Total page views 14,918

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In