MAMIA ya raia wa Kipalestina wameandamana kusherekea kutoroka kwa wafungwa sita waliokuwa wamefungwa katika gereza lenye ulinzi mkali nchini Israel.
Maandamano hayo yamefanyika kuonesha kuwa kitendo cha kutoroka katika gereza lenye ulinzi mkali ni ushujaa kwa raia hao wafungwa hao na kisha kutokomea kusikojulikana.
Washiriki wa maandamano hayo walitangaza mshikamano wao kwa wafungwa hao na wengine wanaodaiwa kushikiliwa kwenye magereza ya Israel.
Wafungwa hao kutoka Palestina ni Zakariya Zubeidi (46), Monadel Yacoub Nafe’at (26), Yaqoub Qassem, Yaqoub Mahmoud Qadri (49), Ayham Nayef Kamamji (35) na Mahmoud Abdullah Ardah (46)
Hata hivyo walifanikiwa kutoroka katika gereza la Gilboa nchini Israel kupitia mashimo ya chini kwa chini baada ya kuchimba handaki kupitia eneo la chooni na kisha kutokea nje kwenye barabara inayopita karibu na gereza hilo kisha kuondoka.
Hadi sasa hatua za vyombo vya usalama vya Israel havitaoa taarifa ya kuwakama wafungwa hao licha ya kuweka ulinzi mkali na vizuizi katika maeneo mengi katika juhudi za kuwasaka na kisha kuwakamata.

Israel leo imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya kile imekitaja kuwa kituo cha kijeshi cha kundi la Hamas kwenye Ukanda wa Gaza baada ya madai kuwa maputo yenye viripuzi yalirushwa ndani ya mipaka ya nchi hiyo.
Taarifa ya jeshi la Israel imesema ndege zake za kivita zimekishambulia kituo cha kuunda maroketi cha kundi la Hamas pamoja na eneo lingine la kijeshi kwenye mji mdogo wa Khan Yunis mashariki mwa Ukanda wa Gaza
Israel imesema eneo hilo lenye Kiwanda cha Saruji na ambalo lipo katikati ya makazi ya watu limekuwa likitumika kuchimba mahandaki yanayotumiwa kufanya vitendo vya kigaidi.
Discussion about this post