TUME ya Uchumi na Jamii ya Umoja wa Mataifa ya Asia Magharibi (ESCWA),imesema asilimia 74 ya idadi ya watu wa Lebanon wameishi katika umaskini mwaka huu wa 2021
ESCWA yenye Makao yake Makuu Beirut, Mji Mkuu wa Lebanoni, imechapisha ripoti ya utafiti inayoitwa “Umasikini Mkubwa nchini Lebanon: Ukweli Unaoumiza na Matarajio Yasiyo na Uhakika” juu ya nchi hiyo katika mtego wa uchumi wenye mgogoro.
Ripoti hiyo, imeonesha kuwa asilimia 74 ya idadi ya watu wa Lebanon wamekumbwa na umasikini mnamo 2021,
Ripoti hiyo ilikumbusha pia kwamba kiwango cha umasikini nchini humo kilikuwa asilimia 55 mwaka 2020 na asilimia 28 mnamo mwaka 2019.
Umaskini wa katika maeneo mengi pia umeathiri asilimia 34 ya idadi ya watu, kulingana na ripoti hiyo, ambapo idadi ya familia ambazo haziwezi kupata huduma za afya nchini zimeongezeka hadi asilimia 33 na wale ambao wana ugumu wa kupata dawa ni zaidi ya asilimia 50.
Tume ya Uchumi ya UN ya Magharibi mwa Asia imetaka kupangwe mipango bora zaidi ya ulinzi wa jamii na kuondoa ukosefu wa ajira na umaskini.
Uchumi wa Lebanon, umekumbwa na misukosuko mingi kutokana na mgawanyiko wa kisiasa kulingana na dini na madhehebu tofauti.
Wakati ESCWA ikitoa ripoti yake,Iran imetuma meli zilizobeba nishati ya mafuta ili kusaidia wananchi kuendelea na kazi zao baada ya nchi hiyo kukumbwa na uhaba mkubwa wa mafuta
Discussion about this post