RIPOTI ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imeonesha kuwa idadi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa akili na kupelekea kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kufikiri, inaongezeka na kufikia watu milioni 55.
Kati ya watu hao milioni 55 asilimia 8.1 ni wanawake na asilimia 5.4 ni wanaume wenye zaidi ya umri wa miaka 65 wanaoishi na shida ya dementia.
Idadi hii inakadiriwa kuongezeka watu milioni 139 ifikapo mwaka 2050.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa Agosti 2,2021 mjini Geneva, Uswisi iliyopewa jina la ‘Hali ya ulimwengu kuhusu hatua za afya ya umma dhidi ya tatizo la kusahau’,
Ripoti hiyo inafafanuwa kuwa ni robo tu ya nchi zote ulimwenguni ambazo zina sera, mkakati au mpango wa kitaifa wa kusaidia watu walio na ugonjwa wa shida ya akili unaosababisha kupoteza kumbukumbu na hali nyingine kama kushindwa kufikiria vizuri.
Mkurugenzi wa WHO, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema, “ugonjwa wa kusahau unawaibia mamilioni ya watu kumbukumbu zao, uhuru na utu, lakini pia unawaibia wao watu wanaowajua na wanaowapenda.
“Ulimwengu unawaangusha watu walio na shida ya akili, na hiyo inatuumiza sisi sote”amesema Ghebreyesus.
Hata hivyo taarifa ya WHO imefafanua kuwa, Ugonjwa wa kusahau husababishwa na magonjwa tofauti tofauti na majeraha ambayo huathiri ubongo, kama ugonjwa wa Alzheimers au hata kiharusi.
Hata hivyo taarifa ya WHO imefafanua kuwa, Ugonjwa wa kusahau husababishwa na magonjwa tofauti tofauti na majeraha ambayo huathiri ubongo, kama ugonjwa wa Alzheimers au hata kiharusi.
Ugonjwa huo unathiri kumbukumbu na kazi nyingine za utambuzi, pamoja na uwezo wa kufanya kazi za kila siku.
Miaka minne iliyopita, serikali mbalimbali duniani zilikubaliana malengo ya wazi ya kuboresha huduma za dementia.
“Lakini malengo pekee hayatoshi, tunahitaji hatua za pamoja ili kuhakikisha kuwa watu wote walio na shida ya akili na kupoteza kumbukumbu wanaishi na msaada na hadhi inayostahili.”amesema Ghebreyesus
Discussion about this post