• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

SMT:Mshirikiane na serikali  kuzuia uharibifu wa mazingira

Bila ushirikiano hakuna mafanikio

by bajeti
December 1, 2021
in Mazingira
0
SMT:Mshirikiane na serikali  kuzuia uharibifu wa mazingira

Viongozi wa Shirika la Maendeleo na Utunzaji wa Mazingira (SMT) Mkoa wa Pwani,wakishangilia leo wilayani Kisarawe muda mfupi baada ya uzinduzi wa ofisi yao wilayani humo (Picha na SMT)

Share on FacebookShare on Twitter

MWENYEKITI wa Shirika la Maendeleo na Utunzaji wa Mazingira Tanzania (SMT) Mkoa wa Pwani Erick Luambano amewataka viongozi kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikiana na serikali kuzuia uharibifu wa mazingira.

Mazingira ni eneo kubwa ambalo lina mambo mengi ikiwemo taka,ukataji miti na uharibifu kutoka vyanzo vya maji na  misitu hali inayopelekea ukame na mabadiliko ya hali ya hewa.

Akizungumza leo wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani na wenyeviti,makatibu na wahasibu wa SMT kutoka wilaya zote za mkoa huo,Luambano amesema ni muhimu kwa viongozi hao kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa ushirikiano ili kufikia malengo makuu ya kuisaidia serikali katika suala zima la mazingira

Amesema mazingira ni pana na ina mambo mengi hivyo serikali pekee haitaweza kumaliza matatizo yanayochangia uharibifu wa mazingira hivyo uwepo wao kisheria utasaidia kupunguza changamoto hizo.

Luambano ameongeza kuwa SMT imesajiliwa kisheria lakini ni muhimu kwa kila mmoja wao kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchi na miongozo kutoka katika Halmashauri husika ili kufikia malengo yao kwa pamoja.

Hata hivyo Luambano amebainisha kuwa SMT inavipaumbele  vyake katika kuhakikisha kuwa utunzaji wa mazingira Mkoa wa Pwani unafanyika kimkakati ili kusaidia vizazi vya sasa na vijavyo.

“Tunakoelekea kila idara lazima itoe taarifa rasmi juu ya kazi iliyofanyika kwa kila baada ya miezi mitatu ili kuongeza ufanisi wa kazi”amesema Luambano

Ameeleza kuwa  majukumu ya kila kiongozi yapo wazi na kwamba vikao ndio vinajenga zaidi katika kuhakikisha kuwa watanzania wanapata maendeleo.

Naibu Katibu wa Shirika la Maendeleo na Utunzaji wa Mazingira (SMT) Mkoa wa Pwani Godfrey Katunzi akichangia mada za utunzaji wa mazingira (mbele ya wajumbe kutoka wilaya zote za mkoa huo hawapo pichani)wakati kikao kazi cha shirika hilo kilichofanyika wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani leo(Picha na SMT)

Kwa upande wake Katibu wa SMT Mkoa wa Pwani  John Naga amefafanua kuwa hadi kufikia sasa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani zimekamilika kwa kuwapata viongozi katika ngazi ya Mwenyekiti wa Wilaya,Makamu Mwenyekiti,Katibu na Katibu Msaidizi akiwemo na mweka hazina.

Amesema mbali na hilo lakini pia wamefanikiwa kupata wakuu wa idara mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanafanya kazi katika fani walizosomea na si vinginevyo.

Naye Naibu Katibu wa SMT Mkoa wa Pwani  Godfrey  Katunzi  amesema utunzaji wa mazingira ndio jambo muhimu kwao kwa sasa kwani kama watanzania ni muhimu kuchukua  hatua zaidi kabla madhara makubwa hayajaikuta nchi.

 

Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo na Utunzaji wa Mazingira (SMT) Mkoa wa Pwani Erick Luambano (katikati) akiwa na viongozi wa SMT kutoka wilaya zote za mkoa huo kabla ya kuanza kwa kikao kazi kilichofanyika wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani leo(Picha na SMT)

Next Post
Majengo kuwekewa mfumo wa umeme kuchajisha magari

Majengo kuwekewa mfumo wa umeme kuchajisha magari

Sea Sense pelekeni elimu Pemba kuwalinda Kasa

Sea Sense pelekeni elimu Pemba kuwalinda Kasa

Kasa ‘Daktari wa bahari’ aliye hatarini kutoweka

Kasa 'Daktari wa bahari' aliye hatarini kutoweka

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 13,061
  • Total page views 14,806

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In