WAKATI dunia ikiendelea na mapambano ya kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa,Uingereza imetangaza kwamba majengo yote mapya yatapaswa kuwa na sehemu za kuchajia magari ya umeme kuanzia mwaka ujao.
Kwa mujibu wa sheria mpya ambayo itatangazwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, inaeleza kuwa majengo mapya yatahitajika kufuata kanuni hiyo kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya waziri mkuu.
Kanuni hizo zitafanikisha kuwepo na sehemu za kuchajia magari 145,000 zaidi ambazo zitafungwa Uingereza kila mwaka mpaka itakapifikia mwaka 2030 wakati ambapo mauzo ya magari yanayotumia mafuta ya Petroli ama Diesel yatasitishwa.
Kanuni hizo pia zitahitajika kwa nyumba mpya na majengo yasiyo na makazi ya watu kama vile maofisi na maduka makubwa ya mahitaji.
Pia itajumuisha majengo yanayofanyiwa ukarabati mkubwa ambayo yatahitajika kuwa na sehemu za maegesho ya magari mpaka 10
Novemba 3 hadi 12,2021 Viongozi kutoka mataifa zaidi ya 200 walikutana huko Uingereza katika mkutano wa kilele wa Mabadiliko ya tabia maarufu kama COP26 ambao ulizikutanisha nchi zenye viwanda vingi na zile zinazoongoza kuzalisha hewa chafu ikiwemo China na Maerekani
Viongozi kutoka zaidi ya nchi 120, zinazowakilisha takriban asilimia 90 ya misitu duniani, waliahidi kusitisha na kubadili ukataji miti ifikapo mwaka 2030.
Pia kulikuwa na ahadi ya methane, iliyoongozwa na Marekani na Umoja wa Ulaya, ambapo zaidi ya nchi 100 zilikubali kupunguza utoaji wa gesi hii chafu ifikapo mwaka 2030.
Wakati huo huo, zaidi ya nchi 40 – ikiwa ni pamoja na watumiaji wakuu wa makaa ya mawe kama vile Poland, Vietnam na Chile – zilikubali kuhama kutoka kwa makaa ya mawe, mojawapo ya jenereta kubwa zaidi zinazozalisha hewa ya kaboni



Discussion about this post