• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Bonde la Mto Kilombero hatarini

by bajeti
June 27, 2022
in Mazingira
0
Bonde la Mto Kilombero hatarini

Shamba la miwa katika Bonde la Mto Kilombero inayotumika kuzalisha sukari(picha kwa hisani ya mtandano)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

 

SHUGHULI za binadamu katika miji ya Lupilo,Ifakara na Mlimba zimesababisha kuchafuliwa kwa Bonde la Mto Kilombero kwa asilimia 80 na  taka ngumu.

Bonde hilo ambalo ni maarufu kwa kilimo cha mpunga na shughuli za uvivi wa samaki linatajwa kuwa ndio eneo la kimkakati katika uzalishaji wa chakula nchini.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Jumla ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Charles Kichere katika Ukaguzi wa Ufanisi kwa kipindi kinachoishia Machi 31, 2022 juu ya udhibiti usiojitosheleza wa uchafuzi ndani ya Mifumo ya Ardhioevu.

Amesema ukaguzi ulibaini kwamba Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), na Halmashauri hazikudhibiti ipasavyo uchafuzi wa mazingira katika mifumo ya ikolojia ya ardhioevu.

Amesema hilo  lilithibitishwa na uwapo wa uchafuzi kutokana na taka ngumu katika maeneo ya ardhioevu manne kati ya nane yaliyotembelewa, ambapo uchafuzi kutokana na taka ngumu ulikuwa kati ya asilimia 0 hadi 80.

Ripoti hiyo ya CAG imefafanuwa kuwa Eneo la Ardhioevu la Bonde la Mto Kilombero lilikiwa na uchafuzi wa juu wa asilimia 80.

“Sababu ya Bonde la Mto Kilombero kuwa na uchafuzi wa kiwango cha juu zaidi kutokana na taka ngumu ni uwapo wa maendeleo ya shughuli za kibinadamu katika Miji ya Ifakara, Mlimba na Lupilo.

“Ukaguzi ulibaini kuwapo kwa uchafuzi kwa majitaka katika maeneo ya ardhioevu yaliyotembelewa ambapo maeneo matano kati ya nane yaliyotembelewa yalionesha uwapo wa uchafuzi wa majitaka.

“Ukaguzi ulibaini kuwa, shughuli za kibinadamu zilichangia kuzuka kwa tatizo la mmomonyoko na kujaa kwa udongo kwenye maziwa na mito kama vile Ziwa Sagara, Ziwa Nyamagoma, Mto Malagarasi, pamoja na kwenye vyanzo vingine vya maji imeongeza ripoti hiyo.

mwisho

Next Post
Wanaume wahanga ugonjwa wa mabusha

Wanaume wahanga ugonjwa wa mabusha

TEF yaungana na wanahabari kupinga sheria kandamizi

TEF yaungana na wanahabari kupinga sheria kandamizi

Waharibu saruji kupinga mradi wa maji

Waharibu saruji kupinga mradi wa maji

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:17
  • Today's page views 17
  • Total visitors 13,276
  • Total page views 15,024

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In