• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Wanaume wahanga ugonjwa wa mabusha

by bajeti
June 29, 2022
in Habari
0
Wanaume wahanga ugonjwa wa mabusha

Mbu wanadaiwa kusababisha ugonjwa wa matende na mabusha

Share on FacebookShare on Twitter

UGONJWA  wa Matende na Mabusha bado haujatokomezwa ambapo kiwango cha maambukizi katika Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi  kiko juu.

Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa  juu ya ugonjwa na Matende na Mabusha.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa Septemba mosi,2013 imeeleza  kuwa zaidi ya  watu milioni 120 duniani kote wameathiriwa na ugonjwa huo wa mabusha na matende na  asilimia 65 ya watu hao wanaishi Kusini Mashariki mwa Asia, wakati asilimia 30 wako barani Afrika na idadi iliyosalia iko katika eneo la tropiki.

Waziri Ummy amesema Mabusha huathiri jinsia zote ingawa kwa asilimia kubwa wanaume ndio wahanga wakubwa.

Hata hivyo wanawake nao hupata Mabusha kwa kiwango kidogo na ili kuweza kuwatofautisha na wanaume ,mabusha kwa wanawake hutambulishwa kwa jina la matende ya sehemu za siri.

Mbali na hilo lakini pia mambukizi ya  vimelea vya ugonjwa wa Matende na Mabusha hutokea kwa jinsia zote ,hivyo hata athari zake hutokea kwa jinsia zote.

“Kwa mujibu wa tathmini iliyofanyika mwaka 2018 kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NMRI)  kupitia mradi wa TakeoFF(Tracking Obstacles to Fight Filariasis) katika Wilaya ya Kilwa,wagonjwa wapatao 1,904 walioathirika na matende na mabusha walitambulika.

“Kati ya hao,wagonjwa 1,143 ambayo ni sawa na asilimia 60 ni wale walioathirika na mabusha tu.

“Wagonjwa 697 ambayo ni sawa na asilimia 36.6 ni wale walioathirika na matende tu,na tathmini ilionesha kuwa asilimia 60 ya wagonjwa hao walioathirika na ugonjwa wa matende ni wanawake,na asilimia 4.4 ni wale walioathirika na matende na mabusha kwa pamoja”ameeleza Waziri Ummy

Waziri Ummy ameongeza kuwa katika utafiti huo hakuna mwanamke aliyetambuliwa kuwa na matende ya sehemu za siri.

“Katika Wilaya ya Kilwa mpaka mwaka 2022 jumla ya wagonjwa 547 wa mabusha wamekwishapata huduma ya upasuaji  wa mabusha na wagonjwa takribani 1,000 wa matende wamepewa mafunzo ya jinsi ya kujihudumia hususani kutunza usafi wa matende”alisema Waziri Ummy

Hata hivyo Waziri Ummy alibainisha kuwa ugonjwa huo unasababishwa na vimelea vya minyoo wadogo wanaoitwa MICROFILARIA wanaosambazwa na mbu

“Microfilaria hao huenda kuishi kwenye tezi(mitoki) na kuanza kushambulia mfumo wa majidamu(Lymphatic system) ambapo ndio tunatapa jina la kitaalamu la ugonjwa huu kuwa ni Lymphatic Filariasis”alisema Waziri Ummy.

mwisho

Next Post
TEF yaungana na wanahabari kupinga sheria kandamizi

TEF yaungana na wanahabari kupinga sheria kandamizi

Waharibu saruji kupinga mradi wa maji

Waharibu saruji kupinga mradi wa maji

WHO:Bidhaa za tumbaku zina kemikali zaidi ya 7000 za sumu

WHO:Bidhaa za tumbaku zina kemikali zaidi ya 7000 za sumu

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In