• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, April 30, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

TEF yaungana na wanahabari kupinga sheria kandamizi

by bajeti
June 30, 2022
in Habari
0
TEF yaungana na wanahabari kupinga sheria kandamizi

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Eliezer Feleshi (katika) akizungumza na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile (kushoto) juu ya mapendekezo ya mabadiliko zinazohusu tasnia ya habari jijini Dodoma hivi karibuni.Kulia ni Mjumbe wa TEF Angela Akilimali(Picha na TEF).

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile ameungana na wanahabari kuhakikisha kuwa sheria zinazoumiza wanahabari zinaondolewa makali.

Hata hivyo TEF imefafanua kuwa chombo hicho kitaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo serikali kuwepo kwa mazingira rafiki kwa wanahabari kutekeleza majukumu yao.

Kauli ya Balile imekuja wakati ambapo wadau mbalimbali wa sekta ya habari wakipendekeza kufanyika kwa marekebisho  katika Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa Mtandaoni ya mwaka 2015.

Akizungumza kwenye semina na wanahabari,jijini Dar es Salaam,Balile amesema wameungana kwa pamoja katika kuhakikisha wanaweka mazingira rafiki kwa wanahabari kufanya kazi zao.

“Kuna sheria nyingi zilizowekwa na kulenga waandishi ama kushambulia tasnia, tumeungana kwa pamoja kuhakikisha sheria hizo zinaondolewa makali yanayoumiuza wanahabari.

“Ni bahati nzuri sasa serikali nayo imeliona hili, mwelekeo wetu una matumaini lakini tunapaswa kuendelea kuwa pamoja mpaka tunafikia lengo,” amesema Balile.

Hata hivyo Kifungu cha 7 (2) (b) cha sheria ya Huduma ya Habari ya Mwaka 2016, inaingilia moja kwa moja uhuru wa mhariri katika kutoa ama kuchapisha habari.

Akitoa ufafanuzi juu ya vifungu katika sheria hiyo, Wakili wa kujitegemea na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) James Marenga, amebainisha kuwa kifungu cha 7 (2) (b) cha sheria hiyo kinapoka mamlaka ya mhariri katika kuamua habari gani ya kuchapishwa.

“Kifungu cha 7 (2) (b) (iv)  cha Sheria ya Huduma za Habari,  kinatoa maelekezo kwa vyombo vya habari binafsi kuchapisha habari zenye umuhimu kwa taifa kwa maelekezo ya Serikali.

Marenga ameongeza kuwa Kifungu hicho cha Sheria kinaingilia uhuru wa uhariri na hasa kwenye vyombo vya habari vya binafsi.

“Kifungu hiki kidogo hakiwezi kufanyiwa marekebisho, tunapendekeza kifutwe”

“Mapendekezo yanakusudia kuwezesha maamuzi ya kihariri kuzingatia vigezo vya taaluma bila kuathiriwa na maamrisho yasiyo ya kitaaluma. Uhuru wa uhariri (editorial independence) utalindwa”amesema Marenga.

Marenga amebainisha kuwa Kifungu cha 7 (3), (a), (b), (c), (f), (g), (h), (i) na (j) vya Sheria hiyo, vinatoa udhibiti wa aina fulani ya habari ama maudhui.

“Mamlaka hii ya kisheria inatoa mwanya kwa serikali kudhibiti taarifa zinazotolewa na vyombo binafsi vya habari.

“Kifungu hiki na vifungu vyake vidogo vinakiuka uhuru wa wa kujieleza bila ya kuwa na sababu za msingi. Hii pia ni kwa mujibu wa maamuzi ya Mahakama ya Haki ya Afrika ya Mashariki (EACJ)”amesema Marenga

Wadau wa habari wanapendekeza kifungu hicho na vifungu vyake vidogo vifutwe kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki. (EACJ).

mwisho

Next Post
Waharibu saruji kupinga mradi wa maji

Waharibu saruji kupinga mradi wa maji

WHO:Bidhaa za tumbaku zina kemikali zaidi ya 7000 za sumu

WHO:Bidhaa za tumbaku zina kemikali zaidi ya 7000 za sumu

Vikombe vya plastiki vyapigwa marufuku

Vikombe vya plastiki vyapigwa marufuku

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:8
  • Today's page views 9
  • Total visitors 15,993
  • Total page views 18,148

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In