NEW DELHI,INDIA
INDIA imepiga marufuku matumizi vikombe vya plastiki ikiwemo kutupwa bidhaa zingine za plastiki kama sehemu ya mpango wa kulinda mazingira.
India yenye watu zaidi ya Bilioni 1.4 imebainisha vitu 19 vya plastiki ambavyo havina umuhimu sana lakini vinaweza kuwa takataka, hivyo kupekelea kusitisha uzalishaji, uagizwaji, usambazaji na uuzaji.
Vitu hivyo ikiwemo vikombe vya plastiki na vijiti vya ice cream pamoja na baadhi ya mifuko ya plastiki itasitishwa na kutakuwepo na mifuko mbadala.
Maelfu ya bidhaa zingine za plastiki kama chupa za maji, soda na mifuko ya chakula, haijajumuishwa kwenye katazo hilo.
Lakini Serikali imeweka malengo kwa wazalishaji kuvichakata tena au kuvitupa baada ya kuvitumia.
Akizungumza na waandishi wa habari nchini humo Waziri wa Mazingira wan chi hiyo Bhupender Yadav amesema marufuku hiyo ilikuwa imetangazwa kwa mwaka mmoja ambapo sasa muda umekwisha.
Kwa upande wake Mratibu wa Kikundi cha Asia-Pasific Satyarupa Shekhar alisema marufuku hiyo ya nchi nzima inajumuisha sio matumizi ya plastiki lakini pia uzalishaji au uagizaji wake
Hata hivyo watengenezaji wa plastiki waliiomba serikali ya nchi hiyo kuchelewesha katazo hilo, kutokana na mfumuko wa bei na upotezaji wa ajira utakaotokea.
Mamilioni ya tani za taka hizo za plastiki huchafua bahari na huathiri wanyamapori ambapo wanasayansi bado wanajaribu kutathmini hatari zinazosababishwa na vipande vidogo vya plastiki .
Utengenezaji wa plastiki hutoa gesi chafu zinazo ongeza joto duniani ambapo India ni nchi yenye viwanda vinavyotengeneza zaidi ya tani 243,000 za taka za plastiki kila mwaka.
Utafiti hivi karibuni,umeonesha kuwa zaidi ya viungio vya kemikali 8,000 vinatumika kwenye usindikaji wa plastiki, na hutoa gesi chafu.
mwisho




Discussion about this post