NA MBARAKA KAMBONA,MWANZA
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itawakopesha wavuvi nchini kote boti za kisasa zaidi ya 150 ili waboresha shughuli zao na kuongeza uzalishaji wa samaki.
Mbali na hilo lakini pia Serikali imetoa kiasi cha Sh,Bilioni 20 ili kuwawezesha watanzania hasa vijana kufuga samaki.
Ulega ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza alipomtembelea nyumbani kwake Spika Mstaafu Pius Msekwa wakati wa ziara yake ya kuhamasisha vijana na makundi mwengine kuchangamkia fursa hiyo.
Amefafanuwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuwatoa wavuvi katika uvuvi wa kuwinda na kufanya ufugaji wa kisasa wa uhakika.
Amebainisha kuwa boti hizo zitafungamanishwa na teknolojia za kisasa zitakazomsaidia mvuvi kurahisisha shughuli za uvuvi.
Ulega amefafanua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuwatoa wavuvi katika uvuvi wa kuwinda na kufanya ufugaji wa kisasa wa uhakika.
Katika hatua nyingine Ulega amefichua kuwa serikali imetoa kiasi cha Sh.Bilioni 20 kwa watanzania na makundi ya mbalimbali wakiwemo vijana ili waweze kufuga samaki katika vizimba vya Ziwa Viktoria.
Hata hivyo Ulega amewataka vijana na makundi mengine kuchangamkia fursa hiyo adhimu..
Kwa upande wake Spika Mstaafu Msekwa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuwezesha vijana kufuga samaki ili wanufaike kupitia uchumi wa buluu.
Msekwa amesema mambo ambayo yanafanywa na Serikali ya Awamu ya Sita hasa kwa kuwezesha vijana kujiajiri ni mambo ambayo Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere alitamani sana kuyafanya na hivyo kama angekuwa hai mpaka leo angefurahi sana.
“Haya yote uliyoyasema Mwl. Nyerere alitamani kuyafanya wakati wa uhai wake, kama angekuwepo leo angefurahi sana kwa sababu yale yote aliyoyataka kuyafanya Rais Samia anayaendeleza kwa kasi kubwa, hongereni sana”, amesema Msekwa




Discussion about this post