• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Geor Davie akabidhi bajaji kumuinua mwanamke kiuchumi.

by bajeti
August 26, 2022
in Habari
0
Geor Davie  akabidhi bajaji kumuinua mwanamke kiuchumi.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa la GeorDavie Ministries International (Ngurumo ya Upako) Geor Davie

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,ARUSHA

KIONGOZI  Mkuu wa Kanisa la  GeorDavie Ministries International (Ngurumo ya Upako) Geor Davie ameendeleza moyo wake wa kutoa misaada ili kuwainua watanzania kiuchumi.

Mbali na kutoa fedha na magari kwa nyakati tofauti lakini pia amekuwa akiguswa na hali waliyonayo baadhi ya waumini wake na wasio waumini wake hivyo kuamua kutoa msaada wake ili kuwasaidia.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Kiongozi huyo alimkabidhi Angela Tarimo pikipiki ya magurudumu matatu (Bajaji) yenye thamani zaidi ya Sh.Milioni saba ambaye aliomba ili aweze kujikwamua kimaisha

Akizungumza mbele ya waumini wake katika Kanisa lake lililopo Kisongo jijini Arusha Geor Davie ametoa sababu pia zilizomfanya kutoa pikipiki hiyo ya magurumu matatu kwa mama huyo wa watoto wawili.

Amesema Angela Tarimo Jumapili iliyopita alikuwa amemuandikia ujumbe akimuomba amsaidie bajaji ili aweze kujikwamua kiuchumi.

Amesema baada ya kuona ujumbe wake aliamua kumwita mbele ya waumini wake ili aeleze sababu ya kuomba Bajaji na endapo ataitapa basi ataiendesha mwenyewe

“Nilimwita mbele yenu,katika mahitaji mengi nilimsimamisha  Angela Tarimo ambaye aliomba mtaji wa bajaji afanye biashara ili aweze kujiajiri mwenyewe,nikamhoji mbele yenu,hivyo leo ninamruzuku Bajaji maana alisema atakuwa anaendesha yeye mwenyewe.

“Aliandika hivyo anajituma na aliponieleza hivyo nikaridhika na nimemruzukua Bajaji na ina vibali vyote na kadi imeandikwa jina lako Angela Tarimo  pamoja na gharama za bajaji na ninachukua nafasi hii  kumkabidhi Angela Sh.500,000 kwa ajili ya mafuta  na ufunguo huu hapa”amesema Kiongozi huyo anayejulikana pia kama Nabii Dkt Geor Davie

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa stakabadhi za bajaji hiyo,funguo na fedha taslimu  za mafuta,Tarimo amesema anashukuru kwa kuwa amemtoa katika umasikini.

“Nashindwa jinsi ya kushukuru baba,ni kweli kwamba umenitoa katika umasikini baba yangu,hakika nitafanya vizuri na ninamuomba mungu anisaidie,nitaingia barabarani na nitaendesha mwenyewe”amesema Tarimo

Awali akizungumza mbele ya wafanyabiashara wadogo jijini Arusha alikokwenda kuwapatia fedha za mitaji ya zaidi ya Sh.Milioni 10,Kiongozi huyo amesema Mungu ndiye amemuongoza kufanya hivyo,kwa sababu watu wadogo hata Kanisani ndio wanaotoa sadaka zaidi kwa kujinyima.

“ Mimi naona ni jambo zuri na la baraka kwa kufanya hivi hasa tunapokuwa tumefanikiwa katika maisha ni vizuri tuwakumbuke watu wadogo tukijua ndiko tulikotoka,na watu wenye uwezo wawakumbuke watu wadogo.

“Watu wadogo kwa kweli ni watu wanafanya kazi mchana na usiku ndio wanajitahidi,ndio wanabeba Taifa hili kwa asilimia kubwa sana,kwa hiyo tuwakumbuke vijana wetu wadogo wainuke.

“Unajua unaweza kutoa 50,000 au 100,000 huwezi kujua itamsaidia kiasi gani yule mtu”alisema Kiongozi hiyo Nabii Geor Davie

Baadhi ya watu waliofanikiwa kupewa magari na Kiongozi huyo ni pamoja na Goodluck Gozbert ambaye alizawadiwa gari mbele ya waumini wa kanisa hilo.

Next Post
Aweso awataka wakuu mabonde ya maji  kulinda vyanzo vya rasilimali hiyo

Aweso awataka wakuu mabonde ya maji kulinda vyanzo vya rasilimali hiyo

Masanja:Wahifadhi jengeni mahusiano mazuri na wananchi kurahisisha kazi zenu.

Masanja:Wahifadhi jengeni mahusiano mazuri na wananchi kurahisisha kazi zenu.

Mchimbaji ajipatia tanzanite ya bilioni 2.24  Mererani

Mchimbaji ajipatia tanzanite ya bilioni 2.24 Mererani

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In