• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Serikali yatoa Bilioni 15 kununua magari ya polisi

by bajeti
August 25, 2022
in Habari
0
Serikali yatoa Bilioni 15 kununua magari ya polisi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya Polisi mkoani Kilimanjaro leo Agosti 25,2022.Picha na Jeshi la Polisi)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,KILIMANJARO

SERIKALI  imetoa kiasi cha Sh.Bilioni 15 ili  kununua magari yatakayopelekwa kwa Makamanda wa Polisi wa mikoa na Wilaya nchini kote.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aosti 25,2022 kwa vyombo vya habari na Afisa Habari wa Jeshi hio Demetrius Njimbwi imeeleza kuwa  kauli hiyo imetolewa leo mkoani Kilimanjaro na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya Polisi, Masauni amesema mbali na serikali kutoa fedha hizo lakini pia imetoa fedha ya mafuta itakayokwenda moja kwa moja wilayani ili kurahisisha utendaji kazi za Polisi.

Hata hivyo Masauni amewataka askari waliohitimu mafunzo hayo kuwaheshimu Watanzania ikiwa ni pamoja na kutenda haki sambamba na kuyashughulikia matukio ya uhalifu kwa wakati na kwa haraka.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura amesema kuwa hadi sasa hali ya nchi ni salama amani na utulivu wa kutosha kwani Jeshi hilo linaendelea kudumisha hali hiyo kwa kushirikiana na wananchi, vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya utoaji haki.

Kwa upande wake Mkuu  wa Shule ya Polisi Tanzania SACP Ramadhani Mungi amesema shule ilipokea zaidi ya wanafunzi 4310 na waliohitimu mafunzo hayo 4122 huku wengine 186 wakiachishwa  mafunzo hayo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu.

Aidha, wahitumu hao wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya nadharia na vitendo.

Next Post
Geor Davie  akabidhi bajaji kumuinua mwanamke kiuchumi.

Geor Davie akabidhi bajaji kumuinua mwanamke kiuchumi.

Aweso awataka wakuu mabonde ya maji  kulinda vyanzo vya rasilimali hiyo

Aweso awataka wakuu mabonde ya maji kulinda vyanzo vya rasilimali hiyo

Masanja:Wahifadhi jengeni mahusiano mazuri na wananchi kurahisisha kazi zenu.

Masanja:Wahifadhi jengeni mahusiano mazuri na wananchi kurahisisha kazi zenu.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In