• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Wananchi watakiwa kutunza vitalu vya miti ili kuhifadhi mazingira

by bajeti
August 22, 2022
in Mazingira
0
Wananchi watakiwa kutunza vitalu vya miti ili kuhifadhi mazingira

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja (wa pili kutoka kulia) akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kali(aliyeinama) kukagua mradi wa kitalu cha miche ya miti kinachosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.(Picha na Ofisi ya Maliasili na Utalii)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU, MAGU

NAIBU  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema amewataka  wananchi kuwa wazalendo katika kulinda vitalu vya miti ili kuhifadhi mazingira.

Masanja ametoa kauli hiyo leo wilayani Magu mkoani Mwanza wakati akikagua mradi wa kitalu cha miche ya miti wenye thamani ya Sh.Milioni 43 unaotekelezwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) .

Amesema ni muhimu kwa wananchi kuwa wazalendo kwa kuitunza miche ya miti watakayokabidhiwa na TFS ili iweze kuleta matokeo chanya ya kuhifadhi mazingira.

“Tuwaombe wananchi miche hii watakapogawiwa waitunze vizuri kwa ajili ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo”amesema Masanja

Ameongeza kuwa  katika utekelezaji wa mradi huo, awamu ya kwanza zimetolewa fedha kiasi cha Sh.Milioni 17 kwa TFS  ambapo Serikali itaendelea kutoa fedha kwa awamu nyingine ili kukamilisha mradi.

Ameongeza kuwa lengo la uanzishwaji wa kitalu hicho ni kupunguza athari za uharibifu wa mazingira hususan katika Mkoa wa Mwanza ambapo kwa sasa utekelezaji wake umeanzia Wilaya ya Magu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kali amesema kupitia kitalu hicho wananchi wa Wilaya ya Magu watanufaika sana kwa sababu miche itapelekwa kwenye maeneo ambayo yalikwishaharibika ili kuyarudisha kwenye asili yake ya awali.

Aidha Kali amewataka wananchi kuitunza na kuilinda miche ya miti watakayokabidhiwa .

“Kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake na kwa wale wafugaji msiingize mifugo kwenye maeneo ambayo tumepanda miti”amebainisha Kali

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) mara baada ya kukagua mradi wa kitalu cha miche ya miti Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza. Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kali.(Picha na Ofisi ya Maliasili na Utalii)

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa TFS  Kanda ya Ziwa, Thomas Moshi amesema kitalu hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha miche laki tatu kwa mwaka, hivyo kuendelea kuihudumia jamii ili kuhakikisha maeneo ambayo hayana miti na uoto wa asili unarudi.

Aidha amefafanuwa kuwa wananchi wanatakiwa kuelimishwa ili waweze kujua faida za miti katika kuleta nishati mbadala, kuleta mvua na pia kutumika kama mitishamba ya dawa za asili.

Kitalu hicho kimefadhiliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Mfuko wa Misitu Tanzania (Taff kwa kushirikiana na TFS.

Next Post
Serikali kuwakopesha wavuvi boti zaidi ya 150.

Serikali kuwakopesha wavuvi boti zaidi ya 150.

Dar es Salaam

Dar es Salaam

Serikali yatoa Bilioni 15 kununua magari ya polisi

Serikali yatoa Bilioni 15 kununua magari ya polisi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 13,056
  • Total page views 14,801

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In