NEW YORK,MAREKANI
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewasili Jijini New York nchini Marekani ambapo anatarajia kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msaidizi wa Makamu wa Rais – Habari jijini Dodoma leo Septemba 19,2022 Franco Singaile amesema Makamu wa Rais anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika Ukumbi wa Mikutano wa Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani tarehe 22 Septemba 2022.
Aidha ameongeza kuwa Makamu wa Rais ataongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano mbalimbali inayohusu Uchumi, Elimu, Afya, Demokrasia na Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo Tanzania imealikwa na nchi washirika, Taasisi za kimataifa na Asasi binafsi.





Discussion about this post