• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Makala

Mchanga;rasilimali ya pili kutumika duniani baada ya maji

by bajeti
September 27, 2022
in Makala
0
Mchanga;rasilimali ya pili kutumika duniani baada ya maji

Wachimbaji wa mchanga

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

MCHANGA ni punje ndogo za mwamba uliosagika kufikia punje ndogondogo  kati ya milimita 0.063 hadi mbili.

Punje hizo zinatokana na mmomonyoko wa mawe makubwa zaidi kama changarawe yaliyosukumwa na upepo au maji kwa mfano mtoni, baharini au kwenye mteremko wa mlima.

Mchanga na changarawe hutumika zaidi katika maendeleo ya dunia hasa katika ujenzi wa majengo,barabara na hata katika viwanda ikiwemo vya saruji.

Hata hivyo uchimbaji wa mchanga na changarawe umeonekana kuwa ni sehemu ya uharibifu wa mazingira kutokana na kuchimbwa bila utaratibu.

Aprili 26, 2022 Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) limeeleza kuwa tani bilioni 50,zanatosha kujenga ukuta wenye upana wa mita 27 na urefu wa mita 27 kuzunguka sayari ya Dunia.

Hiki ni kiwango cha mchanga na changarawe kinachotumika kila mwaka, na kuifanya kuwa rasilimali ya pili inayotumika zaidi duniani kote baada ya maji.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNEP imeeleza kuwa kuwa kuzingatia mchanga unavyotumika unapaswa kutambuliwa kama rasilimali ya kimkakati na uchimbaji na matumizi yake yanahitaji kufikiriwa upya,

Aidha imefafanuwa kuwa mchanga ni rasilimali ya pili duniani kwa matumizi na unapaswa kusughulikiwa viziri  Mabadiliko ya kisheria, nyenzo za ujenzi kutoka kwa vitu vilivyotumiwa, mawe yaliyopondwa na ‘mchanga wa madini’ kutoka kwa uchimbaji wa madini, ni miongoni mwa masuluhisho.

Ripoti hiyo, iliyotolewa na kikosi cha UNEP’s GRID-Geneva, inatoa mwongozo unaohitajika uliokusanywa kutoka kwa wataalamu duniani ya kuanza kutumia mbinu zilizoboreshwa za uchimbaji na usimamizi wa rasilimali hiyo.

Kuchimba mchanga ambako una umuhimu mkubwa kwa mifumo ya ekolojia, kama vile mito, maeneo ya pwani au baharini, kunaweza kupelekea mmomonyoko wa udongo, kuongezeka kwa chumvi kwenye chemichemi ya maji, kupoweza kustahimili mawimbi ya dhoruba na athari yake kwa bayoanuai na kuhatarisha maisha kupitia, usambazaji wa maji, uzalishaji wa chakula, uvuvi, au sekta ya utalii na kadhalika.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mchanga ni sharti utambuliwe kama rasilimali ya kimkakati, sio tu kama nyenzo ya ujenzi, lakini pia kwa kwa kaxi zake mbalimbali kwa mazingira.

Wanasisitiza kuwa serikali, viwanda na watumiaji wanapaswa kuweka bei ya mchanga kwa njia ambayo inatambua thamani yake halisi katika jamii na kwa mazingira.

Kwa mfano, kuweka mchanga ufuoni unaweza kuwa mkakati wa gharama nafuu zaidi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kutokana na jinsi unavyolinda dhidi ya mawimbi ya dhoruba na athari yake kutokana na kupanda kwa kina cha bahari – huduma kama hizo zinapaswa kujumuishwa wakati wa kukadiria bei yake.

Kiwango cha kimataifa kuhusu jinsi ambavyo mchanga unavyochimbwa kutoka kwa mazingira ya baharini pia kinapaswa kuwekwa, ripoti hiyo inapendekeza.

Hii inaweza kuleta mabadiliko makubwa chanya kwani uchimbaji mwingi wa baharini hufanywa kupitia zabuni za umma zilizo wazi kwa kampuni za kimataifa.

Wakati uo huo, ripoti hiyo inapendekeza kwamba uchimbaji wa mchanga kutoka fukweni upigwe marufuku kutokana na umuhimu wake kwa ustahimilivu wa maeneo ya pwani, mazingira na uchumi.

Mkurugenzi wa GRID-Geneva kwa UNEP na mratibu wa jumla wa programu wa ripoti hiyo Pascal Peduzzi amesema ili kufikia maendeleo endelevu, wanahitaji kubadili kwa kiwango kikubwa namna wanavyozalisha, namna tunavyojenga na kutumia bidhaa, na kubadili miundombinu na huduma zeo.

“Rasilimali zetu za mchanga huisha, na tunahitaji kuzitumia kwa njia ya busara.

“Tukielewa jinsi ya kushughulikia nyenzo dhabiti zinazochimbwa zaidi ulimwenguni, tunaweza kuepuka janga na kukuza uchumi unaotumia rasilimali zaidi ya mara moja,” amesema Peduzzi

Mchanga ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na unahitajika kutengeneza saruji na kujenga miundomsingi muhimu kuanzia nyumba,barabara hadi hadihospitali.

Kwa kutoa makazi na maeneo ya kuzaliana kwa mimea na wanyama mbalimbali, mchanga pia una umuhimu mkubwa wa kusaidia bayoanuai, ikijumuisha mimea ya baharini inayoteka kaboni au kuchuja maji.

Rasilimali hiyo ni muhimu ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu na kukabiliana na majanga ya aina tatu kwa sayari ya mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi na uharibifuwa bayoanuai.

Hata hivyo,rasilimali hiyo inatumika kwa kasi kuliko inavyoweza kujitengeneza tena, na kwa hivyo  kuwajibika kuusimamia ni muhimu.

Next Post
Tanzania yashiriki Kombe la Dunia kwa Watu wenye Ulemavu.

Tanzania yashiriki Kombe la Dunia kwa Watu wenye Ulemavu.

Taasisi ya Jai yazitaka halmashauri kutenga fedha kwa wazee

Taasisi ya Jai yazitaka halmashauri kutenga fedha kwa wazee

Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie apongezwa kuisaidia jamii

Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie apongezwa kuisaidia jamii

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In