• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie apongezwa kuisaidia jamii

by bajeti
October 3, 2022
in Habari
0
Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie apongezwa kuisaidia jamii

Kiongozi Mkuu wa Kanisa la GeorDavie Ministries International (Ngurumo ya Upako) GeorDavie

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

ZAIDI ya makanisa 10  jijini Arusha wameunga mkono juhudi za Mch. Daudi Mashimo za kumpongeza Nabii Mkuu Dkt, GeorDavie wa Kanisa la  GeorDavie Ministries International (Ngurumo ya Upako) kupitia matembezi yaliyopewa jina la Ngurumo ya Upako Matembezi Marathoni.

Matembezi hayo yaliyofanyika Oktoba mosi,2022 jijini Arusha kutokana na Kiongozi huyo kusaidia jamii kwa hali na mali ikiwemo kutoa fedha taslimu.

Mbali na kutoa fedha na magari kwa nyakati tofauti lakini pia amekuwa akiguswa na hali waliyonayo baadhi ya waumini wake na wasio waumini wake hivyo kuamua  kuwasaidia kwa kuwapatia mitaji zikiwemo fedha taslimu.

Matembezi hayo yaliyopewa  jina la Ngurumo ya Upako Matembezi Marathoni yaliwajumuisha watu mbalimbali walioguswa na matukio ya kujitoa kwa kiongozi huyo kwa jamii na wengine waliofanikiwa kujikwamua kiuchumi kutokana na misaada ya Nabii huyo.

Kiongozi huyo wa Kanisa mbali na kusaidia jamii lakini pia amekuwa akiunga mkono juhudu za serikali pindi wanapohitaji msaada kutoka kwake.

Baadhi ya taasisi za serikali ambazo zimefaidika na msaada huo ni pamoja na Jeshi la Magereza Mkoa wa Arusha ambapo lilipokea Sh.Milioni 20 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi katika maeneo ya gereza.

Hata hivyo baadhi ya vyama vya siasa navyo havikuachwa katika kupata msaada wa Kanisa hilo la Ngurumo ya Upako.

Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie amekuwa akizungumza ndani ya Kanisa lake lililopo Kisongo jijini Arusha sababu za kutoa misaada hiyo ya kifedha,vyombo vya moto kama magari,pikipiki za magurudumu matatu na misaada mingine ikiwemo kusaidia vituo vya kulelea watoto yatima.

“ Mimi naona ni jambo zuri na la baraka kwa kufanya hivi hasa tunapokuwa tumefanikiwa katika maisha ni vizuri tuwakumbuke watu wadogo tukijua ndiko tulikotoka,na watu wenye uwezo wawakumbuke watu wadogo.

“Watu wadogo kwa kweli ni watu wanafanya kazi mchana na usiku ndio wanajitahidi,ndio wanabeba Taifa hili kwa asilimia kubwa sana,kwa hiyo tuwakumbuke vijana wetu wadogo wainuke”

Kauli hiyo ya Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie aliitoa jijini Arusha wakati akitoa fedha zaidi ya Sh.Milioni 10 kwa wafanyabiashara wa Soko la Kisongo  wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea.

Oktoba mosi ,2022,Makanisa zaidi ya 10 yalishiriki katika kuandaa matembezi ya  kumpongeza Kiongozi huyo kutokana na kusaidia jamii bila ubaguzi.

Katika matembezi ya marathon hiyo yaliyohudhuriwa na waumini wa makanisa mbalimbali ikiwemo wasanii na watangazaji wa vituo vya redio nchini lilionesha jinsi kiongozi huyo anavyodhamini maisha ya walio katika hali ya chini na kuwainua kuichumi.

Akizungumzia kuhusu sababu za pongezi hizo kupitia matembezi,mmoja wa waandaaji wa matembezi haye Mchungaji David Mashimo amesema sababu kubwa ya kuandaa  ni kuguswa na misaada yake kwa jamii bila ubaguzi.

Mashimo amebainisha kuwa wametumia zaidi ya Sh.Milioni 18 kuandaa tamasha hilo ambalo lilihudhuriwa na mamia ya watu wa Jiji la Arusha na mikoa jirani.

“Haya ni matembezi ya pili, ya kwanza tulifanya Dar es Salaam na kutembea kilomita zaidi ya 15 kwa ajili ya kumpongeza na ya pili ni haya ya Oktoba Mosi,2022 hapa katika viwanja vya Mgambo jijini Arusha ili kuendelea kumpongeza”amesema Mashimo

Next Post
Tanzania yaifunga Uzbekistan 2-0

Tanzania yaifunga Uzbekistan 2-0

Dola Bilioni 19.2 kukabili mabadiliko tabianchi

Dola Bilioni 19.2 kukabili mabadiliko tabianchi

Waziri Mchengerwa aitaka Klabu ya Fenerbehche ya Uturuki kuweka kambi Tanzania

Waziri Mchengerwa aitaka Klabu ya Fenerbehche ya Uturuki kuweka kambi Tanzania

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In