• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Taasisi ya Jai yazitaka halmashauri kutenga fedha kwa wazee

by bajeti
October 3, 2022
in Habari
0
Taasisi ya Jai yazitaka halmashauri kutenga fedha kwa wazee

Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Jai na Diwani Mstaafu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Ukonga jijini Dar es Salaam Juma Mwaipopo,akizungumza na Wazee wa Kata ya Zingiziwa iliyopo wilayani Ilala juu ya haki zao kabla ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh.600,000 mwishoni mwa wiki iliyopita(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

HALMASHAURI nchini zimeombwa kutenga fedha za mikopo isiyo na riba kwa Wazee ambao wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Wito huo umetolewa Chanika jijini Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Jai Juma Mwaipopo wakati wa maadhimisho ya siku ya Wazee duniani .

Mwaipopo ambaye amesema hali ya Wazee ni mbaya licha ya kuwa wao ndio waliofanisha maendeleo yanayoonekana sasa.

Amesema Wazee ni hazina ambapo ndani yao kuwa madaktari, wahandisi, mafundi na wenye fani mbalimbali ambao wakikaa pamoja wanaweza kuunda kitu kinachoweza kuwaingizia kipato kutokana na kiwango kidogo wanachopata baadhi yao cha malipo ya uzeeni (Pesheni).

“Nilikuwa Diwani wa Kata ya Ukonga na wakati nilipokuwa hapa niliona jinsi Wazee wanavyotaabika hivyo nilifanikiwa kuanzisha Umoja wao lakini pia nilipofika Zingiziwa kutoa msaada niliambiwa kuna mzee alifariki kwa kula udongo kutokana na njaa.

“Nilihuzunika sana sasa kama mjini wazee wako hivi huko mikoani hali ikoje hivyo mimi ninashauri Halmashauri zote nchini zitenge fedha kwa ajili ya kuwasaidia wazee kama wanavyofanya kwa Watu wenye ulemavu, Wanawake na Vijana”amesema Mwaipopo.

Mwaipopo ameongeza kuwa licha ya Serikali  kuwa na mpango wa TASAF  wa kusaidia Kaya masikini lakini walengwa hawafikiwi na fedha hizo wakiwemo Wazee hivyo kunahitajika mikakati ya kuwasaidia Wazee.

“Wazee sasa hivi ndio wameachiwa mzigo mkubwa wa familia kutokana na vijana wao wengi kukosa ajira hivyo wengi wao wanapokea Sh.100,000 na chini ya hapo hivyo hawawezi kupambana na hali ya maisha ya sasa,ni muhimu kwa Serikali kuwaongezea fedha kama wanavyofanya kwa watumishi wengine wanaoongezwa mshahara”amebainisha  Mwaipopo

 

Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Jai Juma Mwaipopo(Mwenye koti jeuzi katikati) akiwa na Wazee wa Kata ya Zingiziwa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Oktoba mosi,2022 alipokwenda kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo vyakula.(Picha na mpigapicha wetu)

Mwaipopo akiongozana na viongozi wa Jai walifanikiwa kutoa misaada mbalimbali  kwa Wazee wa Kata ya Zingiziwa kwa kuwapatia vyakula mbalimbali ikiwemo mchele, sukari sabuni ambavyo vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh.600,000

Next Post
Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie apongezwa kuisaidia jamii

Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie apongezwa kuisaidia jamii

Tanzania yaifunga Uzbekistan 2-0

Tanzania yaifunga Uzbekistan 2-0

Dola Bilioni 19.2 kukabili mabadiliko tabianchi

Dola Bilioni 19.2 kukabili mabadiliko tabianchi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 13,061
  • Total page views 14,806

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In