• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Vyombo vya habari vyaombwa kuandika habari za Kanisa

by bajeti
September 26, 2022
in Habari
0
Vyombo vya habari vyaombwa  kuandika habari za Kanisa

Kiongozi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba anayejulikana kama BABA HALISI

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

IBADA ni nguzo mojawapo iliyo dhahiri miongoni mwa dini kadhaa katika kuunganisha dhamira za mwenye kushika dini na mhimili wa imani.

Kwa upande wa Kanisa Halisi la MUNGU BABA lenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam kwa upande wa Tanzania chini ya Baba wa Uzao wa MUNGU BABA

Kanisa hili linaloamini katika misingi mitatu ambayo ni AMANI, UPENDO NA UZALISHAJI, limekuwa katika harakati za kumkomboa mwanadamu kiroho na kimwili kwa maana ya kutoishi maisha ya umasikini.

Mbali na hilo lakini pia  linaamini kuwa ili waumini wake waweze kuishi maisha ya kumsifu MUNGU BABA, limekuwa likihimiza kila mmoja kushiriki shughuli za uzalishaji mali ili kufuta Umasikini, Ufukara, Ombaomba na hali ya kuwa Tegemezi.

Linaamini, ili waumini wake waweze kuishi maisha ya kumsifu MUNGU BABA, limekuwa likihimiza kila mmoja kushiriki shughuli za uzalishaji mali ili kufuta Umasikini, Ufukara, Ombaomba na hali ya kuwa Tegemezi.

Hivyo, kupitia misingi hiyo waumini wa kanisa hilo wamekuwa wakipata fursa ya kuonesha maonesho ya bidhaa wanazotengeneza ili kujiinua kutoka katika wimbi la Umasikini kwa njia halali.

Hadi sasa, waumini wa Kakisa hilo wameshapata fursa ya kuonesha bidhaa zao zaidi ya mara nne kupitia eneo la Kanisa hilo ambalo mamia ya waumini wake hutumia fursa hiyo kujifunza mbinu sahihi zaidi za kupambana na umasikini katika familia zao

Kanisa hilo limekuwa likiendelea kupanua shughuli zake katika mikoa mbalimbali nchini  ili kuhakikisha kuwa waumini wao wanaondokana na hali ya umasikini katika kuhakikisha kuwa wanafanyakazi kazi kwa bidii ili kujieletea maendeleo

Kanisa hilo  ambalo sasa lina vituo zaidi ya 15 ikiwemo nchi za Afrika Mashariki na Kati ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DCR) ,Rwanda,Burundi,Kenya, na Nchi zingine za Afrika Mashariki ambapo chanzo chake ni Tegeta jijini Dar es Salaam na kusambaa katika mataifa hayo tofauti na makanisa mengine ambayo huanzia nje ya nchi na kuingini nchini,

Baadhi ya Viongozi wa Serikali ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kushangazwa na mfumo wa Kanisa hilo.

Kazi nyingine kubwa inayofanywa na Kanisa Halisi la Mungu Baba ni kuhimiza upendo miongoni mwa jamii ili kujenga Taifa lenye mshikamano na umoja.

Wakati hayo yakifanyika na Kanisa hilo,Kiongozi wa Kanisa hilo amevitaka vyombo vya habari kuandika habari za Kanisa kwa kuwa hata wao wanauhubiri habari za maendeleo kwa jamii.

Ujumbe wa Kiongozi huyo ni muhimu kwa jamii hasa ya vizazi vya sasa vinaendana na sayansi na teknolojia ili kuifikia kasi ya dunia.

Ikiwa vyombo vya habari vitaandika kwa kina jinsi makanisa kama haya yanavyosaidia waumini wao kuondokana na umasikini basi watakuwa wameisaidia Serikali katika kupambana na ukosefu wa ajira kwa wengine wao wanaweza kujiari kupitia mifumo ya Kanisa lao na kujiingizia kipato

Vyombo vya habari vimekuwa vikiangalia sana masuala muhimu hasa wakati wa sherehe ambazo hualikwa kwa viongozi ndipo nasaha za viongozi hao zinapoandikwa kwa uzito lakini nje ya mfumo huo hakuna habari za viongozi wa dini zinazopewa uzito ilhali wakati mwingine ujumbe wao unaweza kuwa msaada katika jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 26,2022 jijini Dar es Salaam Kiongozi wa KANISA HALISI LA MUNGU BABA,BABA HALISI amesema mara nyingi waandishi wa habari hawapendi kuandika habari za Kanisa kwa sababu wanaamini kuwa ni za kidini na kiimani au za tumaini la vitu ambavyo havitakuja vitokee.

“Mimi mara nyingi naomba tu nisema ni kweli ni Kiongozi wa Kanisa lakini mara nyingi tunaongelea habari za maendeleo na uchumi  na msiwe mnaogopa kuandika habari za Kanisa hili kwa sababu ukiangalia hata mahubiri tunayohubiri,tunahubiri maendeleo na uchumi.

“Ni kweli tunazungumzia kumletea matunda Chanzo Halisi lakini mahali tunapoanzia ni lazima kwanza tumuinue mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu ya moyo wa Taifa,yeye akiwa ni  Kiongozi wa Taifa na kitabu kinaniambia kwamba anao huo moyo wa Taifa.

“Sasa usipomuinua yeye moyo wa Taifa hujafanya kitu chochote hivyo tunaanzia hapo kwa mujibu wa Timotheo 1:2-4,na hapo utaona tayari tunazungumzia suala la kitaifa na maendeleo”amesema BABA HALISI.

Aidha ameongeza kuwa huwezi ukasema wewe ni muhubiri lakini ukaacha kuzungumzia kitu kinachohusiana na watu wakati unahubiria watu hivyo wao hawazungumzii tu habari za ibada lakini pia habari za maedeleo kwa jamii.

Next Post
Mchanga;rasilimali ya pili kutumika duniani baada ya maji

Mchanga;rasilimali ya pili kutumika duniani baada ya maji

Tanzania yashiriki Kombe la Dunia kwa Watu wenye Ulemavu.

Tanzania yashiriki Kombe la Dunia kwa Watu wenye Ulemavu.

Taasisi ya Jai yazitaka halmashauri kutenga fedha kwa wazee

Taasisi ya Jai yazitaka halmashauri kutenga fedha kwa wazee

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In