NA MWANDISHI WETU,DODOMA
WANANCHI waliovamia Hifadhi ya Msitu wa Bondo uliopo katika Kijiji cha Mswaki,Kata ya Msanja wilayani Kilindi Mkoa wa Tanga wametakiwa kuondoka ndani ya hifadhi hiyo ifikapo Desemba 30,2022.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt.Pindi Chana, wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilindi Omar Mohamed Kigua bungeni jijini Dodoma leo Septemba 19,2022.
Amesema Serikali imeweka matangazo ya kuwataka wananchi wote kuondoka ndani ya hifadhi hiyo ifikapo Desemba 30,2022. .
“Kwa nyakati tofauti hifadhi hii imekuwa ikivamiwa kwa ajili ya shughuli za kibinadamu zikiwemo kilimo,makazi na kuchungia mifugo” amesema Masanja .
Aidha, amebainisha kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali misitu nchini.




Discussion about this post