• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Dk.Mpango kuongoza mazungumzo na wawekezaji kuhusu miradi ya kimkakati Ivory Coast

by bajeti
November 1, 2022
in Habari
0
Dk.Mpango kuongoza mazungumzo na wawekezaji kuhusu miradi ya kimkakati Ivory Coast

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Mipango na Maendeleo wa Ivory Coast Kaba Nialé mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Félix Houphouët Boigny jijini Abidjan nchini humo Oktoba 31,2022. (Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye anaiwakilisha pia Tanzania nchini Ivory Coast Dkt.Benson Bana).(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais Dkt.Philip Mpango amewasili jijini Abidjan nchini Ivory Coast ambapo atamwakilisha Rais  Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Uwekezaji Barani Afrika litakalofanyika Novemba 2-4. 2022.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 31,2022 kwa vyombo vya habari na Msaidizi wa Makamu wa Rais – Habari Franco Singaile amesema Makamu wa Rais amewasili nchini humo Oktoba 31,2022.

Amesema akiwa nchini humo anatarajia kuongoza mazungumzo baina ya Tanzania na wawekezaji mbalimbali kuhusu uwekezaji katika miradi ya kimkakati nchini Tanzania katika Sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji, Usafirishaji na Uchukuzi.

Amesema Jukwaa la Uwekezaji Barani Afrika linaratibiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na waanzilishi wa Jukwaa hilo na linalenga kuwakutanisha Wawekezaji, Sekta Binafsi na Sekta ya Umma ili kuweka mikakati ya kufadhili miradi endelevu.

Aidha amebainisha kuwa Jukwaa hilo linashirikisha Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, Wakuu wa taasisi na mashirika ya kimataifa pamoja na wafanyabiashara.

Next Post
Kikosi cha Kuratibu Usafishaji Mito na Mabonde chakabidhi taarifa ya Mto Msimbazi

Kikosi cha Kuratibu Usafishaji Mito na Mabonde chakabidhi taarifa ya Mto Msimbazi

Ivory Coast

Dkt.Mpango:Tanzania ni sehemu sahihi ya kuwekeza

Dkt.Mpango:Tanzania ni sehemu sahihi ya kuwekeza

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 13,061
  • Total page views 14,806

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In