• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Serikali:Mpango wa Uchumi wa Bluu utasaidia mapambano athari za mabadiliko ya tabianchi

by bajeti
November 17, 2022
in Mazingira
0
Serikali:Mpango wa Uchumi wa Bluu utasaidia mapambano athari za mabadiliko ya tabianchi

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis akishiriki uzinduzi wa Programu ya Utekelezaji wa Uchumi wa Bluu kwa nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania kupitia Benki ya Dunia uliofanywa wakati wa Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) unaofanyika Sharm El Sheikh nchini Misri(Picha na Ofisi Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Share on FacebookShare on Twitter

CAIRO,MISRI

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis amesema kuanzishwa kwa Programu ya Uchumi wa Bluu kwa Afrika itachochea upatikanaji wa fedha za kusaidia katika mapambano dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesema Serikali imejumuisha masuala ya hifadhi ya mazingira katika Uchumi wa Bluu ili kuhakikisha unakuwa endelevu kwa manufaa ya jamii ya Tanzania.

Khamis amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Programu ya Utekelezaji wa Uchumi wa Bluu kwa nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania kupitia Benki ya Dunia uliofanywa wakati Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) unaofanyika Sharm El Sheikh, Misri.

Amesema Tanzania imejaliwa kuwa na ukanda wa pwani wenye urefu wa takriban kilomita 1,450 kwa urefu ambao unatoa fursa kwa wananchi kujishughulisha na shughuli za uchumi wa bluu kwa vitendo zikiwemo uvuvi.

Aidha Khamis ameongeza kuwa  eneo hilo linachukua takriban asilimia 15 ya ardhi yote ya Tanzania ambapo takriban watu milioni nane wananufaika nalo hivyo, Serikali imeweka utaratibu wa kusaidia utekelezaji wa ajenda ya uchumi wa bluu.

Alizitaja hatua hizo kuwa ni kuanzishwa kwa Wizara Maalum ya Uchumi wa Bluu Zanzibar, kuanzisha Sera na Mkakati wa Maendeleo Uchumi wa Bluu Zanzibar na Mkakati wa Uchumi wa Bluu Tanzania Bara.

“Uchumi wa bluu unatarajiwa kuchochea matumizi makubwa ya rasilimali za maji na maeneo ya pwani, hata hivyo, changamoto za kimazingira zinazosababisha mabadiliko ya tabianchi na uvuvi haramu huenda zikahatarisha au kudhoofisha matarajio ya ukuaji wa uchumi wa bluu,” amesema Khamis

Hata hivyo,aliishukuru Benki ya Dunia (WB) kupitia Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) ambao umesaidia kutokomeza vitendo vya uvuvi haramu.

Naibu Waziri Khamis aliongeza kuwa mradi huo umesaidia na kuimarishwa kwa ulinzi wa makazi ya samaki na matumbawe ya baharini ambapo awali kulifanyika uvuvi haramu uliochangia uharibifu wa makazi na viumbe hai.

 

 

Next Post
Wasimamizi vyombo vya habari vya China,Afrika wakutana Kenya

Wasimamizi vyombo vya habari vya China,Afrika wakutana Kenya

Serikali yazitaka nchi za SADC kudhibiti   uchomaji holela wa taka unaosababisha  sumu ya uPOPs

Serikali yazitaka nchi za SADC kudhibiti uchomaji holela wa taka unaosababisha sumu ya uPOPs

Makamishna wa Tume za Uchaguzi kutoka nchi tisa wakutana Dar es Salaam

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:17
  • Today's page views 17
  • Total visitors 13,276
  • Total page views 15,024

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In