• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Saturday, May 2, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Makamishna wa Tume za Uchaguzi kutoka nchi tisa wakutana Dar es Salaam

by bajeti
November 22, 2022
in Habari
0

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacobs Mwambegele akifungua mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo makamishna/wajumbe wapya na maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa SADC (ECF-SADC) na kuhusisha wajumbe wapya wa Tume za Uchaguzi na maafisa kutoka nchi tisa wanachama wa Jukwaa la ECF-SADC ambazo ni Zambia, Eswatini, Ushelisheli, Botswana, Namibia, Zimbabwe, Lethoto, Malawi na Tanzania ambayo yameanza leo Novemba 22,2022 jijini Dar es Salaam. (Picha na NEC).

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

JUKWAA la Tume za Uchaguzi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (ECF – SADC) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wameandaa mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo Makamishna wapya na maafisa waandamizi wa Tume  ambazo ni wanachama wake.

Mafunzo hayo yaliyoanza leo Novemba 22,2022 jijini Dar es Salaam yanatarajiwa kumalizika Novemba 25, mwaka huu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacobs Mwambegele amesema nchi tisa wanachama wa Jukwaa la ECF-SADC ambao ni Zambia, Eswatini, Ushelisheli, Botwana, Namibia, Zimbabwe, Lesotho, Malawi na Tanzania wanashiriki mafunzo hayo.

Aidha Jaji Mwambegele amesema  baadhi ya nchi ikiwemo Afrika Kusini zitashiriki katika mafunzo hayo kwa njia ya mtandao (Virtually).

Amesema wajumbe  na maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ambayo yatawasaidia katika kuboresha utekelezaji wa majukumu yao.

“Washiriki watajifunza na kubadilishana uzoefu wa namna ambayo  uchaguzi umekuwa ukifanyika katika nchi zao na kuona changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza na namna ya kuzitatua,”amesema Jaji Mwambegele.

Aidha Jaji Mwambegele ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa amezitaja mada zitakazowasilishwa katika mafunzo hayo kuwa ni pamoja na demokrasia, uchaguzi na menejimenti ya uchaguzi, vigezo vya  kimataifa vya upimaji  wa uchaguzi na wajibu wa kuendesha chaguzi za kidemokrasia; Usimamizi wa uchaguzi: Tafsiri, mifano, majukumu na  na nguvu ya kisheria.

“Mada nyingine ni pamoja na Mifumo ya Uchaguzi, Mzunguko wa Uchaguzi, Kalenda ya Uchaguzi na Mipango ya Uchaguzi, Matumizi ya  TEHAMA katika chaguzi,   Masuala yanayojitokeza katika usuluhishi wa migogoro ya uchaguzi na utoaji haki za katika uchaguzi na Uandikishaji wa wapiga kura.

“Pia zipo mada za Siku ya Uchaguzi (Kupiga kura) na Menejimenti ya Matokeo, Changamoto kwa Tume za Uchaguzi, Uongozi wa Tume za Uchaguzi, Utendaji kazi na Uendelevu wake, Ushawishi kwa Wadau wa Uchaguzi, Changamoto na Uhusiano na Tume, Kuendesha Uchaguzi Jumuishi kwa kuzingatia  Jinsia, Vijana na Watu wenye Ulemavu”amefafanua Jaji Mwambegele

Jaji Mwambegele amezitaja mada zingine kuwa ni pamona na Menejimenti ya  Mashinikizo ya Kisiasa, Kugharamia Uchaguzi na Tume za uchaguzi,Ushirikiano kati ya Tume za Uchaguzi na Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya nje ya Taasisi pamoja na masuala yanayojitokeza katika sekta ya mawasiliano ya kidigitali.

Aidha ameongeza kuwa mada zingine ni zile za   kukabiliana na majanga na kujenga uwezo wa namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza na usalama wakati wa uchaguzi, vurugu na namna ya kutatua changamoto pia zitatolewa.

“Baada ya kupatiwa mafunzo ni matarajio kuwa watendaji hawa watakwenda kuhakikisha kuwa chaguzi zinakuwa huru, za haki na zenye kuaminika na hii itasaidia katika kukuza demokrasia itakayochochea amani, usalama na ustawi wa wananchi na Taifa”amebainisha Jaji Mwambegele.

 

 

Next Post
Dkt.Mpango awataka wataalamu,wawekezaji kujadili rasilimali za fukwe kuongeza mchango wake kiuchumi

Dkt.Mpango awataka wataalamu,wawekezaji kujadili rasilimali za fukwe kuongeza mchango wake kiuchumi

Jeshi la EAC kuwasambaratisha waasi wa M23

Jeshi la EAC kuwasambaratisha waasi wa M23

Dkt.Mpango ataka masharti ya mikopo kuangalia upya

Dkt.Mpango ataka masharti ya mikopo kuangalia upya

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:10
  • Today's page views 10
  • Total visitors 16,035
  • Total page views 18,193

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In