• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Jeshi la EAC kuwasambaratisha waasi wa M23

by bajeti
November 24, 2022
in Habari
0
Jeshi la EAC kuwasambaratisha waasi wa M23

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Luanda nchini Angola Novemba 23,2022.

Share on FacebookShare on Twitter

LUANDA,ANGOLA

JESHI la Jumuiya ya Afrika Mashariki limewekwa katika hali ya utayari kuyakabili makundi yote ya waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) likiwemo kundi maarufu la M23 ikiwa yatagoma kuweka chini silaha zao ifikapo Novemba 25,2022

Uamuzi huo umetangazwa Novemba 24,2022 nchini Angola mara baada ya kikao kilichoongozwa na Rais wa Angola Joao Lourenco na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi, akiwemo Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye na  na mjumbe wa amani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye ni Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Mkutano wa viongozi hao umetoa amri ya kusitishwa mapigano ifikapo Novemba 25,2022 saa 12:00 jioni na makundi yote ya waasi wenye silaha hasa la M23 wanaodai kwamba wanapigania haki za watu kutoka kabila la Watutsi Mashariki mwa DRC, kuondoka katika miji ambayo linashikilia ukiwemo mji wa Bunagana.

Taarifa hiyo aidha imesema, waasi watapewa ulinzi na Jeshi la DRC, Jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO) endapo watajisalimisha.

Wanajeshi wa Kenya na Burundi tayari wapo nchini DRC huku Uganda ikitarajiwa kutuma wanajeshi 1000 wiki ijayo.

Maamuzi hayo yamekuja siku chache baada ya aliyekuwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kusema kwamba Rais wa Rwanda Paul Kagame, anayetuhumiwa kuunga mkono waasi wa M23, ameahidi kushawishi waasi hao kuacha vita.

Rwanda imewakilishwa kwenye mkutano huwa wa Novemba 23,2022 na Waziri wa Mambo ya Kigeni  Vincet Biruta.

Serikali ya Rwanda imekuwa ikituhumiwa na Serikali ya DRC kuwa inawaunga mkono na hata kuwasaidia kijeshi waasi wa M23, tuhuma ambazo Kigali imekuwa ikizikanusha.

 

Next Post
Dkt.Mpango ataka masharti ya mikopo kuangalia upya

Dkt.Mpango ataka masharti ya mikopo kuangalia upya

Mtoto wa miaka sita aokolewa akiwa hai chini ya kifusi

Mtoto wa miaka sita aokolewa akiwa hai chini ya kifusi

Mabalozi kushuhudia uzinduzi wa sarakasi

Mabalozi kushuhudia uzinduzi wa sarakasi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In