NA MWANDISHI WETU
CHAMA cha Sarakasi Tanzania (CHASATA) kimeandaa uzinduzi wa kuinua vipaji vya mchezo huo utakaofanyika Novemba 26,2022 jijini Dar es Salaam ambapo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao wamealikwa
Katika uzinduzi huo ukaofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam utaambatana na vikundi vingine ambavyo vitafanya maonesho ya sanaa ya ngoma za asili na sarakasi kikiwemo cha Dragon Acrobatic group, Happy Centre, Shule ya sèkondari ya Hazina na kikundi cha ngoma za asili cha Mlonge Culture troup.
Akizungumzia uzinduzi huo na waandishi wa habari leo Novemba 25,2022 jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa chama hicho Selemani Pembe amesema mbali ya kutambulisha sarakasi kwa jamii pia itatoa nafasi kwa vijana wanaotaka kujifunza mchezo huo kujiandikisha na kupewa mafunzo ya sarakasi katika vikundi hivyo.
Amesema maandalizi ya onesho hilo yamekamilika na mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali wamealikwa ambapo linategemea kuanza majira ya saa 12 jioni hadi saa 3:00 usiku.
Hata hivyo Pembe amebainisha kuwa kila mtanzania anaruhusiwa kufika na hakutakuwa na kiingilio kwani sarakasi ni sanaa kama zilivyo zingine.





Discussion about this post