• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Dkt.Mpango:Viongozi wa dini saidieni kulea vijana kimaadili ili Taifa liwe kwenye mikono salama

by bajeti
November 28, 2022
in Habari
0
Dkt.Mpango:Viongozi wa dini  saidieni kulea vijana kimaadili ili Taifa liwe kwenye mikono salama

Viongozi wa dini mbalimbali nchini,wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango (hayupo pichani) jijini Dar es Salaam Novemba 28,2022 wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania lililofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Viongozi wa dini zote, wakiwemo wa Kimila na Wazee hapa nchini kusaidia kulea watoto na vijana kimaadili ili kuweka mustakabali wa taifa na watu wake kwenye mikono salama.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Novemba 28,2022 jijini Dar es Salaam wakati alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania.

Amesema vijana  wakifundishwa mila na desturi sahihi na kushika mafundisho ya dini, na wakawa na hofu ya Mwenyezi Mungu, maovu mengi yatapungua hapa nchini.

Dkt.Mpango amefafanua kuwa  Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Dini zote katika kujenga maadili mema ndani ya jamii ya watanzania.

Aidha amewasihi viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa, viongozi na watumishi wa Serikali bila kuchoka ili kutekeleza vema mipango ya maendeleo ya nchi na watu wake.

Aidha amekemea vikali ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto wa kike na kiume hapa nchini na kuviagiza vyombo vya dola kuongeza nguvu katika kupambana na ukatili huo.

Amewataka pia walezi na wazazi kuweka mifumo imara ya ulinzi kwa watoto katika ngazi ya familia, mtaa, mashuleni, madrasa, vyuoni na sehemu nyingine ili kulinda haki na ustawi wa watoto na kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyofanyika dhidi yao.

Dkt.Mpango amewakumbusha viongozi wa dini hapa nchini kukemea vitendo vya Rushwa na Ufisadi kupitia nyumba za ibada pamoja na kuwaelimisha wananchi madhara ya kutoa na kupokea rushwa na kushiriki kuhujumu mali za umma.

“Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya utoaji huduma ili kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi pamoja na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo hivi bila kujali cheo au nafasi yake katika jamii”amebainisha Dkt Mpango

Dkt.Mpango amewasihi wazazi na walezi kwa pamoja kushiriki katika mapambano ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya  kwa kutoa elimu kwa jamii pamoja na kutoa taarifa na kuwafichua wote wanajishughulisha na biashara hiyo haramu inayoathiri afya za vijana hapa nchini.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewaasa  Viongozi wa dini  kujiepusha na migogoro ndani ya Taasisi zao ambayo imekuwa ikisababishwa  na uchu wa madaraka, ubinafsi, uchu wa fedha, matumizi mabaya ya mali za taasisi za dini na ukiukwaji wa katiba za taasisi za dini.

Amewahimiza viongozi hao wa dini kusuluhisha mapema migogoro ndani ya taasisi zao inapojitokeza  kwa kuzingatia sheria, miongozo na taratibu zinazokubalika ili wawe mfano mzuri wa maadili kwa jamii ya watanzania.

Kwa Upande Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema Wizara hiyo imeanzisha mfumo wa usajili na usimamizi wa jumuiya hpa nchini unaolenga kusaidia changamoto mbalimbali ambazo zilikua zikilalamikiwa ikiwemo ucheleweshaji wa usajili Jumuiya pamoja na kutopata taarifa mbalimbali.

Mwenyekiti wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Sheikh Alhad Mussa Salum amesema wataendelea kushirikiana na serikali katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili uliopo hapa nchini.

Awali akisoma Risala Katibu Mkuu, Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Mchungaji Dkt. Israel Maasa amesema Jumuiya hiyo imeweza kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kumaliza migogoro mbalimbali kati ya wakulima na wafugaji, kupambana na mila potofu pamoja na kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na Watoto.

Next Post
TBA watakiwa kutekeleza miradi inayozingatia ubora na gharama nafuu

TBA watakiwa kutekeleza miradi inayozingatia ubora na gharama nafuu

CCM:Shahada ya Udaktari kwa Rais Samia ni matokeo ya kazi  kubwa aliyoifanya  kwa  watanzania

CCM:Shahada ya Udaktari kwa Rais Samia ni matokeo ya kazi kubwa aliyoifanya kwa watanzania

Naigeria yaondoa kiingereza kufundishia shule za msingi

Naigeria yaondoa kiingereza kufundishia shule za msingi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In