• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

TBA watakiwa kutekeleza miradi inayozingatia ubora na gharama nafuu

by bajeti
November 30, 2022
in Mazingira
0
TBA watakiwa kutekeleza miradi inayozingatia ubora na gharama nafuu

Baadhi ya Nyumba 3,500 za Watumishi wa Umma zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) katika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewataka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhakikisha kuwa Miradi ya Ujenzi wanayotekeleza inazingatia ubora,gharama nafuu.

Mbali na hilo lakini pia miradi hiyo wanayotekeleza ni muhimu ikawa na tija kwa wapangaji pamoja na ujenzi wa kisasa unaoendana na wakati ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Makamu wa Rais amesema hayo leo Novemba 30, 2022 wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 3,500 za Watumishi wa Umma zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma.

Amesema ni vyema TBA kufanya mapinduzi makubwa ya kiutendaji, kuongeza ubunifu na kujenga misingi mizuri ya kujiendesha kibiashara ili kuweza kupata mapato zaidi na kujiendesha pasipo kutegemea ruzuku kutoka serikalini.

Hata hivyo Dkt.Mpango ameitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuharakisha mchakato wa marekebisho ya kanuni ya Uanzishwaji wa Wakala wa Nyumba Tanzania ili Taasisi iweze kukamilisha taratibu zote za kuingia ubia na wawekezaji hali itakayopunguza utegemezi wa ruzuku ya Serikali pekee katika kutekeleza miradi mikubwa nchini na kutatua changamoto ya kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi hiyo.

Dkt.Mpango amefafanua kuwa Uwekezaji katika Sekta ya ujenzi ni miongoni mwa vipaumbele muhimu vya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo inaendelea kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kama ilivyopangwa.

Aidha ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono ubunifu na mipango ya Taasisi kama TBA kuwa na miradi mingi zaidi ya ujenzi ili kuongeza makusanyo ya ndani na kupunguza utegemezi wa ruzuku kutoka Serikalini.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema mradi huo utapunguza changamoto kubwa ya makazi ya watumishi wa umma waliopo jijini Dodoma pamoja na  ukuzalisha ajira kwa wananchi wanaozunguka mradi huo.

Prof. Mbarawa ameongeza kuwa ujenzi wa mradi huo unasaidia  Wataalamu wazawa wa fani za ujenzi kujengewa uwezo wa taaluma kwa vitendo pamoja na kusaidia kuendelea kukua kwa kasi kwa jiji la Dodoma lililopangwa vizuri kwa kuzingatia mipango miji , kuongezeka kwa mapato ya serikali na huduma za kijamii katika jiji hilo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Daud Kandoro (mwenye fimbo) wakati akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Nyumba 3,500 za Watumishi wa Umma zinazojengwa na TBA katika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma leo Novemba 30,2022.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Awali akitoa taarifa za ujenzi wa mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daudi Kandoro amesema tayari serikali imetoa gharama za utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi huo kiasi cha Sh. Bilioni 14.3 pamoja na kutoa Sh.Bilioni moja katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo wa nyumba nyingine 150 ambapo maandalizi yake yameshaanza.

Kandoro Amesema TBA inaendelea kutekeleza miradi mingine nchi nzima kwa fedha za ruzuku na makusanyo ya ndani ikiwemo mradi wa ujenzi wa nyumba mpya 20 za Viongozi katika eneo la Kisasa Dodoma, ukamilishaji wa nyumba za majaji kwenye Mikoa ya Kilimanjaro, Mtwara, Shinyanga, Tabora na Kagera, ukarabati wa nyumba za makazi ya watumishi wa Umma na Viongozi Tanzania Bara ili kuwawezesha kuishi katika mazingira bora.

Kandoro ameitaja miradi mingine kuwa ni Ujenzi wa Nyumba za Makazi kwa Watumishi wa Umma katika eneo la Magomeni Kota na Temeke Kota, Ujenzi wa jengo la makazi eneo la Masaki, ujenzi wa nyumba 13 za watumishi mikoani, umaliziaji wa jengo la makazi la ghorofa 11 lenye uwezo wa kuchukua familia 22 Mtaa wa Simeoni Arusha.

Next Post
CCM:Shahada ya Udaktari kwa Rais Samia ni matokeo ya kazi  kubwa aliyoifanya  kwa  watanzania

CCM:Shahada ya Udaktari kwa Rais Samia ni matokeo ya kazi kubwa aliyoifanya kwa watanzania

Naigeria yaondoa kiingereza kufundishia shule za msingi

Naigeria yaondoa kiingereza kufundishia shule za msingi

Kigahe:Wafanyabiashara tumieni teknolojia mbadala kukabili mabadiliko ya tabia nchi

Kigahe:Wafanyabiashara tumieni teknolojia mbadala kukabili mabadiliko ya tabia nchi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In