• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Dkt.Mpango awataka wataalamu,wawekezaji kujadili rasilimali za fukwe kuongeza mchango wake kiuchumi

by bajeti
November 23, 2022
in Mazingira
0
Dkt.Mpango awataka wataalamu,wawekezaji kujadili rasilimali za fukwe kuongeza mchango wake kiuchumi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza pamoja na waratibu wa Jukwaa la Nane la Maendeleo Endelevu lenye dhima ya Usimamizi Madhubuti wa Fukwe kwa Maendeleo Endelevu mara baada ya kufungua Jukwaa hilo linalofanyika Jijini Mwanza leo Novemba 23,2022.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewataka wataalamu na wawekezaji kujadili kwa pamoja namna bora ya kutunza, kusimamia na kuwekeza katika rasilimali adhimu za fukwe zilizopo nchini ili kuongeza mchango wake kwenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Novemba 23, 2022 jijini Mwanza wakati akifungua Jukwaa la Nane la Maendeleo Endelevu lenye dhima ya Usimamizi Madhubuti wa Fukwe kwa Maendeleo endelevu.

Amesema unahitajika ubunifu katika kutumia  zaidi ya kilomita 1400 za ukanda wa Pwani ya bahari na fukwe safi, hifadhi tatu za baharini,maeneo tengefu ya baharini 15, maziwa na mito mikubwa ambayo kwa pamoja inaongeza idadi kubwa ya fukwe ambazo  bado hazijaweza kutumika kikamilifu kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Aidha Dkt Mpango amesema serikali ya awamu ya sita imeweka mkazo katika kuendeleza Uchumi wa Buluu pamoja na suala la hifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.

Ameongeza kwamba dhamira ya Serikali ni kuharakisha maendeleo endelevu ya taifa kwa kuzingatia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inayolenga kufikia uchumi jumushi wa Taifa lenye kipato cha kati na maisha bora kwa kila Mtanzania.

Mbali na hilo lakini pia pia ameagiza kila Mkoa, kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, pamoja na wadau wengine kujipanga na kuharakisha mchakato wa kuandaa mpango mkakati utakaoainisha namna ya kufanya uwekezaji wa kuendeleza fukwe zilizopo nchini pamoja na bustani za kupumzikia.

Makamu wa Rais amewasihi viongozi wa mikoa kutekeleza suala la upandaji miti kwa ufanisi ikiwemo ufuatiliaji wa miti hiyo kuhakikisha inafanikiwa kukua kama ilivyopangwa na kuweka malengo yanayotekelezeka  ikiwemo kuwatumia wakala wa misitu nchini (TFS) katika elimu sahihi ya miti itakatokuwa rafiki wa vyanzo vya maji na mazingira.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa Jukwaa la Nane la Maendeleo Endelevu lenye dhima ya Usimamizi Madhubuti wa Fukwe kwa Maendeleo Endelevu mara baada ya kufungua Jukwaa hilo linalofanyika Jijini Mwanza leo Novemba 23,2022.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Awali akitoa taarifa za kuhusu kongamano hilo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) Kadari Singo amesema kongamano limelenga kujadili fursa zilizopo katika uwekezaji wa fukwe kama kichochezi cha maendeleo, changamoto zinazohusiana na utunzaji na usimamizi na uwekzaji wa fukwe pamoja na mifumo ya kisera, kisheria na kitaasisi inayohusiana na usimamaizi wa fukwe nchini.

Singo ameelezea dhima ya mwaka huu katika kongamano hilo kuwa inalenga kufungua majadiliano katika kuelekea kupata suluhisho la namna Madhubuti ya kusimamia na kuwekeza katika fukwe za bahari, maziwa na mito nchini ili ziweze kutoa tija katika ukuaji wa uchumi hapa nchini.

“Dhima imezingatia dhamira ya dhati ya serikali inayolenga kuimarisha uchumi wa nchi pasipo kuharibu mazingira”amefafanua Singo

 

Next Post
Jeshi la EAC kuwasambaratisha waasi wa M23

Jeshi la EAC kuwasambaratisha waasi wa M23

Dkt.Mpango ataka masharti ya mikopo kuangalia upya

Dkt.Mpango ataka masharti ya mikopo kuangalia upya

Mtoto wa miaka sita aokolewa akiwa hai chini ya kifusi

Mtoto wa miaka sita aokolewa akiwa hai chini ya kifusi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In