NAIROBI,KENYA
SHIRIKA Kuu la Utangazaji la China (CMG) Afrika limeandaa semina ya wasimamizi wa vyombo vya habari vya nchi hiyo na Afrika yenye kauli mbiu ya “China na Dunia katika Safari Mpya”
Semina hiyo ambayo imefanyika jijini Nairobi, Kenya,iliwahusu wasimamizi wa vyombo vya habari na wataalam zaidi ya 60 kutoka nchi 20 za Afrika zikiwemo Kenya, Rwanda, Tanzania, Madagascar, Sudan Kusini, Zambia na Sierra Leone
Katika semina hiyo ambayo majadiliano ya kina yalifanyika juu ya ajenda kama “China katika safari mpya ina maana gani kwa Afrika”
Majadiliano mengine yamefanyika juu ya mada “safari mpya ya kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika inakwenda wapi” na “ushirikiano wa vyombo vya habari vya China na Afrika utaleta nini kwa jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya pande hizo mbili”.
Washiriki wamekubaliana kuwa maendeleo mapya baada ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China yatatoa fursa mpya kwa Afrika, na pia ni injini mpya kwa ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika, na kwamba ushirikiano wa vyombo vya habari vya China na Afrika una nguvu kubwa ambazo hazijatumiwa ipasavyo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sera ya Afrika nchini Kenya Profesa Peter Kagwanja amesema kwenye hotuba yake kuwa China inatafuta maendeleo kwa amani, kitu ambacho kinaendana na maslahi ya watu wengi.
Amesema Afrika na China zote zina ustaarabu wenye historia ndefu, zote zilikuwa na historia ya kuteswa na nchi za magharibi, na zote zinakabiliwa na suala la maendeleo.




Discussion about this post