NA MWANDISHI WETU DODOMA
SERIKALI imesema kwa sasa Tanzania haipo tayari kutumia mbegu zilizofanyiwa mabadiliko ya vinasaba maarufu kama GMO na kwamba itajenga maabara mbili kwa ajili ya kuendelea kujifunza ili kuliepusha Taifa kutumia wasichokijua.
Msimamo huo wa Serikali umewekwa wazi na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe jijini Dodoma Januari 10,2022 wakati akizungumza na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Aidha amebainisha kuwa mbegu za pamba za GMO zinazotumiwa na baadhi ya nchi jirani huzalisha nusu ya pamba inayozalishwa kwa kila ekari moja inayovunwa Tanzania kwa kutumia mbegu bora za asili zilizofanyiwa utafiti na watanzania
Hata hivyo Waziri Bashe ameongeza kuwa wizara itaendeleza tafiti za mbegu ili kuzalisha mbegu bora jambo linaonyesha mafanikio makubwa katika matumizi yake.
“Kwa sasa Tanzania haipo tayari kutumia mbegu zilizofanyiwa mabadiliko ya vinasaba lakini itajenga maabara mbili kwa ajili ya kuendelea kujifunza ili kuliepusha taifa kutumia wasichokijua”amesema Bashe
GMO ni mazao yenye vinasaba vilivyoundwa baada ya mbegu kufanyiwa uhandisi jeni ambapo inadaiwa kuwa mazao yaliyoundwa na vinasaba vilivyofanyiwa uhandisi jeni yanatajwa kuwa na athari kwa viumbe hai wakiwamo binadamu, wanyama hata mazingira.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe(aliyechuchumaa),akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Andrew Massawe (Kulia) na Naibu Katibu Mkuu wake, Gerald Mweri wakati wa kikao kazi kati ya Wizara ya Kilimo na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dodoma Januari 10,2023. Picha na mpigapicha wetu.
Katika hatua nyingine Wizara ya Kilimo imetangaza nafasi za mafunzo kwa vijana kati ya miaka 18 hadi 40 yatakayofanyika Jijini Dodoma tatizo la ajira kwa Vijana na kuboresha na kukuza kilimo nchini ili kuwa cha kibiashara,
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Andrew Massawe imeleza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa Ajenda 10/30 chini ya Programu ya Kuwezesha Ushiriki wa Vijana katika Kilimo Biashara (BBT-YIA) yatakayofanyika kwa miezi miwili kuanzia Februari 15, yakitarajiwa kuongeza ajira kwa vijana kufikia milioni tatu ifikapo mwaka 2030.
“Kupitia BBT,Wizara inaratibu uanzishwaji wa mashamba makubwa ya pamoja (Block Farms) kwa ajili ya vijana ,Mradi huu utatekelezwa nchi nzima na vijana wote wenye sifa watapata fursa ya kufanya kilimo biashara katika mnyororowa thamani
“Kwa kuanzia ,Wizara imetambua mashamba yenye jumla ya ekari 162,492 katika Wilaya ya Chunya(Mbeya),Bahi na Chamwino(Dodoma),Misenyi na Karagwe(Kagera),Uvinza na Kasulu(Kigoma)
“Wizara inatangaza fursa za mafunzo ya Kilimo Biashara kwa awamu ya kwanza kwa vijana katika Kituo cha Mafunzo ya Kilimo Bihawana mkoani Dodoma,vijana watapatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na baada ya mafunzo hayo ,wahitimu watakabidhiwa mashamba kwa ajili ya kilimo kwa utaratibu na masharti yatakayoanishiwa na ili kupata nafasi hii vijana wanatangaziwa kuomba kujiunga na mafunzo hayo kupitia halmshauri husika kuanzia Janauri 10-30,2023”ilibainisha taarifa hiyo




Discussion about this post